Maafisa biashara kutoka mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida wakifuatilia mafunzo ya sheria ya leseni za biashara yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) yanayofanyika katika ukumbi wa JK convetion Centre jijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA ) Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa Maafisa Biashara wa mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida yanayofanyika kwa wa siku tano jijini Dodoma.
Na mwandishi Wetu, Dodoma
MAAFISA biashara nchini wametakiwa kutambua kuwa
jukumu lao kuu ni kuwezesha ufanyaji wa
biashara badala ya kuwa wakusanya mapatato shughuli ambayo ni sehemu tu ya kazi
ambayo wanatakiwa kuifanya.
Akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo ya sheria za leseni za biashara kwa maafisa biashara
wa mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro, yanayofanyika jijni Dodoma, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey
Nyaisa amesema Maafisa Biashara
wanapaswa kutumia sheria pia kutumia busara wakati wa utekelezaji wa majukumu
yao na kwamba ikiwa watazifunga biashara wasitarajie mfanyabiashara huyo
kufanya biashara na badala yake watachangia kuua uchumi wa nchi.
“Muepuke
sana kufunga biashara, afisa biashara kazi yako kubwa ni kusimamia wafanyabiashara,
ikiwa utaifunga biashara utasimamia watu gani, hii ina maana huwataki
wafanyabiashara “, alisema Bw. Nyaisa na kuongeza kuwa anatarajia kuwa mafunzo hayo yatasaidia
kubadili fikra na mitizamo ya maafisa biashara na watendaji wengine wa serikali
na kuwa watoa huduma na msaada kwa
wafanyabiashara, hivyo ni vema wakafuatilia mafunzo hayo vizuri ili
watakaporudi katika vituo vyao vya kazi watumike kama chachu ya uwekezaji, ukuaji na uanzishwaji wa
biashara.
Bw. Nyaisa
amesema, kila mmoja awe kipimo kwa kuwezesha watu kuanzisha na kufanya biashara
ili ifikapo mwisho wa mwaka kila mmoja ajipime na kujihoji ni watu wangapi
aliowawezesha kuanzisha biashara, wawafuate watu na kuwawezesha kuanzisha
biashara na sio watu wawafuate wao kutaka
kuanzisha biashara na wasiwe watu wanaokimbiwa na wafanyabiashara.
Sambamba
na hilo maafisa biashara hao wametakiwa kutoa huduma bora na kwa weledi jambo ambalo litawezesha wafanyabiashara walio wengi kurasimisha
biashara kupata fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali ama taasisi mbalimbali
za kifedha.
Amesisitiza kuwa maafisa biashara wana jukumu la kuwaelimisha wafanyabiashara kutambua umuhimu wa kusajili biashara zao na kupata leseni pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa wafanyabiashara hao ili kuendelea kukuza uchumi wa nchi.
Amewataka
wafanyabiashara kuondokana na dhana kwamba gharama ya usajili wa majina ya
biashara na makampuni kubwa
jambo ambali si kweli kwani BRELA ni taasisi ya huduma na gharama
zinazotozwa ni ndogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...