Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Alhaj Othman Masoud Othman, amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kujitahidi kuwa na malezi mema kwa vijana wao,  kwani kufanya hivyo kutasaidia sana nchi kupata viongozi bora, wacha Mungu na waadilifu.

Alhaj Othman ameyasema hayo leo Msikiti wa Amaan Uwanjani Mjini Unguja, alipowasalimia waumini wa dini ya kiislamu, mara baada ya swala ya Ijumaaa.

Alhaj Othman, amesema viongozi wema na bora wanatokana na wananchi ndani ya jamii, na maandalizi yake ni malezi bora yanayozingatia msingi sahihi ya ucha Mungu, jambo linalopaswa kuzingatiwa sana, hivyo amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kutokujisahau katika kutimiza jukumu lao la malezi bora kwa watoto.

Aidha amewaasa wazazi kuwa na tahadhari kubwa juu ya matumizi mabaya ya simu hasa kwa watoto wa kike, kwani imekuwa ni chanzo kikubwa cha kuharibika kwa maadili ya watoto hao.

Mapema Khatibu wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti huo wa Amaan Uwanjani Sheikh Idrissa  Omar, amewakumbusha waumini wa dini ya kiisalamu kuwa wacha Mungu wa kweli na kujiweka mbali na matendo maovu yanayomchukiza Mwenyezi Mungu.

Amesema vitendo vya Shirki na zinaa ni miongoni mwa madhambi makubwa ambayo waislamu wanapaswa kujiepusha nayo na kujenga jamii ya uadilifu na yenye kumcha Mungu.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...