Na Mwandishi wetu, Hanang’
MBUNGE
wa viti maalum wa Vijana Taifa kupitia Mkoa wa Manyara, Asia Halamga,
amekamilisha mbao za upauzi wa nyumba mpya ya Katibu wa Jumuiya ya Umoja
wa Vijana UVCCM Wilaya ya Hanang’ baada ya kukabidhi mbao 214.
Asia
amekabidhi mbao hizo baada ya kuzindua rasmi jana Hanang’ Vijana
Jogging Club ambapo alikuwa mgeni rasmi wa mazoezi hayo yaliyoanzia
ofisi za ofisi za CCM Wilaya mji mdogo wa Katesh na kuishia uwanja wa
shule ya msingi Katesh.
Akizungumza
wakati akikabidhi mbao hizo Asia amesema katika hatua ya upauaji
zilikuwa zinahitajika mbao 214 na akaonelea azunguke kwa wadau
mbalimbali wa maendeleo ili kukamilisha lengo la upauzi wa nyumba hiyo.
Amesema
alikutana na mdau wa maendeleo wa mjini Babati, Emmanuel Khambay ambaye
alijitolea mbao 104 za kupaulia na yeye akamalizia hizo 110 za
kukamilisha upauaji.
“Hapa
ni nyumbani na kila ninapokuwa nakuja sipendi kuja patupu nakuja na
jambo fulani na jambo hilo ndiyo hili la kukamilisha mbao za ujenzi wa
nyumba ya mtumishi wa UVCCM Hanang’,” amesema Asia.
Amesema
ili nyumba hiyo ikamilike inapaswa kupauliwa kwa mabati na mifuko
kadhaa ya saruji hivyo wadau wengine wa maendeleo hasa vijana wanapaswa
kushiriki kuikamilisha.
Mwenyekiti
wa UVCCM Wilayani Hanang’ Yohane Leonce amemshukuru Asia kwa moyo wa
kujitolea kwa kuwaunga mkono katika kufanikisha maendeleo hasa ujenzi wa
nyumba hiyo.
“Kwa
niaba ya vijana wa Hanang’ tunakushukuru na kukupongeza kwa kujitolea
kutuunga mkono katika ujenzi wa nyumba ya katibu wetu wa UVCCM Hanang’,”
amesema Leonce.
Mdau
wa maendeleo wa mjini Babati, Emmanuel Khambay amesema akiwa mzaliwa wa
mkoa wa Manyara, anajivunia kuwaunga mkono vijana hao kwa kutoa mbao
hizo 104.
Khambay
amesema wataendelea kuungana mkono katika kufanikisha maendeleo kwani
Manyara itajengwa na wana Manyara wenyewe na siyo vinginevyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...