Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
DIWANI
wa Kata ya Mbwewe Halmashauri ya Chalinze ,Mkoa wa Pwani Omary Msonde,
amewaagiza walimu Sekondari Changarikwa kuacha tabia ya kuwarudisha
wanafunzi nyumbani wanaodaiwa pesa ya chakula, badala yake wazazi
wawajibishwe.
Aidha
amewaonya wazazi na walezi wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao wa
kuwalipa fedha za chakula, akisema kwamba watawaita kwenye kikao maalumu
kuzungumzia suala hilo.
Msonde
ametoa agizo hilo baada ya kurudishwa shuleni hapo wanafunzi
walioondolewa kwa kukosa pesa za chakula, ambapo alisema awali wanafunzi
wanaodaiwa pesa hizo walirudishwa nyumbani kabla ya kurejea shule
kuendelea na masomo yao, huku akiwataka ambao hawajaripoti wafanye hivyo
mapema.
"Tumewarejesha
shule watoto asilimia 80 ya waliorudishwa nyumbani kwa kukosa pesa za
chakula, uamuzi huo uliochukuliwa na uongozi wa shule haukuwa sahihi
kwani mwanafunzi hausiki na utafutaji wa pesa, jukumu lake ni kusoma
hivyo kumfukuza shule ni kumwonea," alisema Msonde.
Alieleza
kuwa alipopata taarifa za kufukuzwa kwa wanafunzi hao alikutana na
uongozi wa shule, na Kata wakazungumzia suala hilo, tayari agizo hilo
limeshatekelezwa ambapo wanafunzi asilimia 80 wamesharejea shuleni, huku
akiagiza waliosalia waripoti haraka.
"Sanjali
na hilo pia nimeagiza uongozi wa shule uwasiliane na wazazi wa
wanafunzi ambao bado hawajaripoti wafike shule maramoja, pia waandae
kikao na wazazi au walezi wa wanafunzi ambao wanadaiwa pesa za chakula
wazungumzie suala hilo," alisema Msonde.
Aidha
ameshangazwa kuwepo kwa madeni hayo kwa wanafunzi husika pasipokuitwa
wazazi wao kuzungumzia, mpaka kufikia kiwango kikubwa hali ambayo kwa
namna moja au nyingine inamrudisha nyuma kimasomo mwanafunzi husika.
"Nimewaambia
walimu na ofisa elimu kwamba ni marufuku kuwarudisha nyumbani
wanafunzia wanaodaiwa pesa ya chakula, badala yake wazazi waitwe
ikiwezekana wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na si kumfukuza
mwanafunzi," alisema Diwani huyo.
Mmoja
wa wazazi aliyejitambulisha kwa jina la Asha Sizya amemshukuru diwani
huyo, huku akielezea masikitiko yake kutokana na mtoto wake kukaa nyumba
kwa wiki mbili kwa sababu ya yeye kukosa pesa ya chakula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...