Charles James, Michuzi TV


TUNASHUKURU! Wananchi wa Kata ya Idete Jimbo la Mlimba, Morogoro wamemshukuru Mbunge wa Jimbo hilo, Godwin Kunambi kwa kukabidhi kiasi cha Sh 220,000 kwa uongozi wa Zahanati ya Kata hiyo kwa ajili ya kufanikisha uungwaji wa Bomba la Maji mserereko.

Kwa muda mrefu Zahanati hiyo imekua haina maji ya mserereko jambo ambalo lilikua linawalazimu wagonjwa wanaoenda kupata huduma hasa akina Mama wajawazito kulazimika kutumia bomba la kumpampu jambo ambalo kwao siyo rafiki.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kiasi hicho cha fedha na Mbunge Kunambi, Afisa Muuguzi wa Zahanati hiyo, Juliana Marko amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada wake huo ambapo amesema utawasaidia sana akina Mama wajawazito ambao wamekua wakienda kujifungulia kwenye Zahanati hiyo.

"Tumekua na changamoto hii ya Maji kwa mrefu ambapo imekua ikitulazimu sisi na wagonjwa wetu kutumia bomba la kupampu lakini kwa kiasi hiki cha fedha ambacho kimetolewa na Mbunge wetu Kunambi tuna uhakika Sasa wa kuwa na bomba la maji mserereko ambalo litakua msaada kwetu, tunatumia nafasi hii kumshukuru sana," Amesema Juliana.

Kwa upande wake Mbunge Kunambi akikabidhi mchango huo wa kufanikisha uungwaji wa Maji kwenye Zahanati hiyo amesema lengo lake ni kuona anapunguza changamoto ya Afya kwenye Kata hiyo ambapo tayari pia ameshafanikiwa kupatikana kwa Afisa Tabibu ambaye amesharipoti huku pia akiahidi kumalizia jengo la Mama na Mtoto ndani ya kipindi cha miezi sita.

" Nimefika hapa kukagua ujenzi wa jengo hili la Mama na Mtoto lakini nikaambiwa kuwa hapa hakuna Maji Mserereko haiwezekani Zahanati ikose bomba la maji, natoa kiasi cha fedha kinachotakiwa na nikuagize Mhandisi wa Maji wa Wilaya kuhakikisha ndani ya siku mbili hizi Bomba linafika na maji yanatoka hapa.

Sera ya Serikali ni kuona kila Kata inakua na Kituo Cha Afya, Sisi Jimbo letu lina Kata 16 lakini mpaka sasa tuna Vituo vinne vya Afya tunataka ndani ya miaka mitano hii tuwe na vituo takribani 10, hivyo nikuagize Diwani wa hapa Idete uhakikishe eneo linapatikana ili na sisi hapa tuanze ujenzi wa Kituo chetu cha Afya," Amesema Kunambi.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo ametembelea Kata ya Mofu ambayo imekua ikikabiliwa na changamoto ya umeme ambapo amejionea nguzo za umeme zikiwa zimeshafika kwenye kata hiyo ambapo alimpigia Simu Meneja wa Tanesco Wilaya ya Kilombero ambaye amemuahidi hadi kufikia Desemba Mwaka huu Kata hiyo itakua inawaka umeme.

" Niwaombe Tanesco ni kweli nguzo zimeshafika lakini tunahitaji mtuongezee nguzo zingine kwa ajili ya kupeleka umeme kwenye  maeneo ya huduma za Jamii ikiwemo Shule ya Sekondari na Zahanati yetu ya Mofu lakini pia kwenye kaya maskini," Amesema Kunambi.

 

Hili ni jengo la nyumba ya watumishi wa Zahanati ya Mofu ambapo Mbunge Kunambi wa Jimbo la Mlimba amefika kujionea hatua za ujenzi wake.
Mbunge Godwin Kunambi wa Jimbo la Mlimba akikagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto kwenye Zahanati ya Idete ambayo utekelezaji wa Ujenzi huo unafanywa na Ofisi ya Mbunge kwa kushirikiana na wananchi wake.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mkoani Morogoro, Godwin Kunambi akimkabidhi kiasi cha Sh 220,000 Afisa Muuguzi wa Zahanati ya Idete kwa ajili ya kufanikisha uwekwaji wa Maji ya Bomba la Mserereko kwenye Zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi akiwa ameongozana na Viongozi wa CCM Kata ya Idete na watendaji wa Serikali ametembelea Zahanati ya Kata hiyo kujionea maendeleo yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...