NA MWANDISHI WETU.

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge amewaalika wawekezaji wa ndani na nje kwenda mkoani humo kuwekeza kwenye eneo la viwanda kwani mkoa una sifa zote za kuwekeza.

Alizitaja sifa hizo kuwa ni pamoja na ardhi ya kutosha, usalama, kijiografia Pwani iko katika enmeo lenye miundombinu ya kuwezesha bidhaa zizlizozalishwa viwandani kufika kwa urahisi sehemu yoyote kwanin ni karibu na bandari lakini pia miundombinu ya barabara nayo iko vizuri.

Mheshimiwa Kunenge aliyasema hayo Agosti 3, 2021 wakati wa ziara ya kukagua kiwanda cha kuzalisha sukari cha Bagamoyo Sugar Ltd kinachomilikiwa na mwekezaji mzalendo Said Salim Bakhresa.

Alisema Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, imeshaweka wazi kuwa wawekezaji waje kuwekeza nchini kwani serikali imeweka mazingira mazuri na wezeshi ya kumfanya muwekezaji afaidike na uwekezaji wake.” Alisisitiza

Naye mratibu wa mradi huo, Bw.  Sufian Ally, Ameeleza kuwa  Serikali iliwapatia  Ekari 25,000  Mwaka 2016 na kwa awamu hii wamelima hekta 1330 na ifikapo Julai 2022 wataanza Kuzalisha sukari. Kazi za Ujenzi wa Kiwanda  zimekamilika kwa asilimia 95.

Ameeleza kuwa kwa  awamu hii ya kwanza Kiwanda kitatoa ajira kwa watu 1,500 na utakapo kamilika utaajiri watu 8,000.

Mhe. Kunenge  amepongeza uwekezaji huo, "Ni Uwekezaji Mzuri na sisi katika Mkoa wa Pwani ni mradi wa mfano na miradi hii mikubwa kwa mkoa huu ni miradi yangu ninaifuatilia mwenyewe" alisema Kunenge.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...