Mtanange wa utangulizi wa ufunguzi Tamasha la Kizimkazi 2021 kati ya
wenyeji Kizimkazi Mkunguni FC dhidi ya Mtende FC ilipigwa jana jioni
katika dimba la Mgombewa, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, ambapo
wenyeji hao walitamba nyumbani kwa kuwachabanga mabao 3-0 wana Mtende
FC. Mchezo huo na mingine mingi itakayoendelea ni sehemu ya michuano kuelekea maadhimisho ya siku ya Tamasha
la Kizimkazi hapo Agosti 28, 2021 lililo dhaminiwa na Benki ya CRDB na kufanyika Mkoa wa
Unguja Kusini, Zanzibar. Mchezo huo ulikuwa ni wa kuvutia na wenye hisia kali kwa kila upande, vibweka pia havikukosekana.
Beki wa Timu ya Kizimkazi Mkunguni FC akiwa ameruka juu kumdhibiti Mshambuliaji wa timu ya Mtende FC wakati mtanange huo uliopiga jana jioni katika dimba la Mgombewa, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar
Vumbi lilitimka kweli kweliiii....
Vyenga kama vyote, jamani kuna vipaji hukuuuu..... Wale Aseno kama vipi waje tu huku kujichagulia.... (Utani kidogo)
Daktari wa Timu akienda kutoa huduma ya kwanza kwa mchezaji wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...