Mlundikano
wa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari madarasani umeonekana
kurudisha nyuma kampeni ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO 19
mashuleni hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi hao.
Uchunguzi
uliofanywa na Blog hii umebaini kuwa baadhi ya shule hazichukui
tahadhari za kuwalinda wanafunzi na mambukizi ya UVIKO licha ya serikali
kusisitiza mara kwa mara wananchi kuchukua tahadhari.
Dk.Jairy
Khanga ni mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma ambapo amewataka
maafisa elimu pamoja na ,walimu Mkoani humo kuendelea kufata muongozo
wa udhibiti wa maambukizi wa UVIKO 19 katika shule za Msingi na
sekondari ,vyuo na taasisi za elimu uliotolewa julai mwaka huu na
kuwasimamia wanafunzi ili waweze kuchukua tahadhari ya maambukizi hayo
hasa wakiwa mashuleni.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii,Dk.Khanga alisema,jukumu la kutoa elimu i la
wadau wote na tayari wataalam wa afya walitoa mafunzo kwa maafisa
elimu ambao wanapaswa kuwasimamia wanafunzi mashuleni wakati wote
ili kuwakinga na maambukizi hivyo walimu na walezi wanapaswa kuendelea
kuwasaidia wanafunzi kuchukua tahadhari .
Kwa
Upande wake Mwanafunzi shule ya Msingi Ally Juma alisema mlundikano
Darasani ni mkubwa hakuna nafasi ya mita moja pia hata wasiponawa mikono
au kutovaa barakoa walimu hawawaulizi hivyo wanaona kama hakuna ugonjwa
wa UVIKO19.
"Hatunawi
mikono ,waa hatuvai barakoa tulivaa tulipofungua tu shule lakini sasa
hivi tunaendelea kusoma bila mashariti mimi naona kama ugonjwa umeisha ,
kwani zamani wazazi walituzuia kwenda shule na kushika vitu na kila
muda walimu na hata wazazi majumbani walisema tunawe mikono na kutuzuia
kucheza kwenye mikusanyiko"alisema Mariam
kwa
upande wake Mwanafunzi Faraja Batazar mwanafunzi ruhila shule ya
Msingi aisema mlundikano madarasani ni mkubwa na wanafunzi hawavai
barakoa bali wanaendelea na masomo yao ya kila siku ambapo amekuwa
akijifunika kitambaa pindi akikumbuka kuwa kuna ugonjwa huo.
"wanafunzi wacheza ,wanashikana mikono bila kunawa hivyo tunaweza kuambukizwa UVIKO 19 , tunaomba walimu watusaidie"alisema
Kwa
upande wake Ofisa elimu Mkoa wa Ruvuma Emmanuel Kisongo amekiri kuwepo
kwa mlundikano mkubwa wa wanafunzi na kuwa baadhi ya shule zimekuwa
hazichukui tahadhari ambapo amewataka kuendelea kuchukua tahadhari ya
kujilinda na UVIKO 19
Aliongeza
kuwa Jukumu la kutoa elimu mashuleni ni la Wizara ya ya afya ila
wataendelea kuwaelimisha watoto kujilinda na ugonjwa huo kipindi chote
wanapokuwa shuleni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...