Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi wa shule za St. Mary’s Mutta Rwakatale ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwasimamia watoto na kuhakikisha kuwa wanakuwa katika maadili mema sambamba na kuwapatia elimu ikiwa ni haki yao kwa mujibu wa sheria.

Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa wamahafali ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo yaliyofanyika  kwenye shule ya St Mary’s Mbagala mkoani Dar es Salaam, ambapo alisema kumpatia elimu mtoto kunamsaidia asiwe tegemezi baadae.

Amesema kila mzazi anajukumu la kuhakikisha kuwa anamuelimisha mwanaye kwa hali yoyote ile ili atakapokuja kuwa mkubwa aweze kumsaidia na kusisitiza kuwa watoto wanahaki ya kusikilizwa katika mahitaji yanayowasaidia kutimiza malengo yao.

“Mtoto anapokuomba umpeleke kwenye masomo ya ziara wakati wa likizo, umnunulie daftari, kalamu na vitu vingine vinavyomsaidia katika masomo yake jitahidi umpatie kwani mafanikio yake ni furaha kwetu sisi walimu kwenu wazazi na kwake pia, watoto ndio viongozi, madaktari, marubani walinzi na nguvukazi ya taifa kwa baadae tuwalinde na kuwarithisha elimu bora.

“Tuwe na tabia ya kuwajenga watoto watu kiimani tukifanya hivyo watakuwa na hofu, wengine ni wakorofi lakini tukiwa na kawaida ya kuongea nao kwa kuwaelekeza taratibu watakuelewa,” alisisitiza.

Aliwataka wazazi pia kuwasisitiza wanafunzi hasa wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa kuhitimu wiki mbili zijazo kuhakikisha kwamba wanasoma kwa bidii ili watimize malengo yao.

Aidha,, watoto wanategemewa na familia na taifa kwa ujumla hivyo wanapaswa kujilinda na kuwa na tahadhari wasijihusishe na makundi mabaya mitaani wanaporudi nyumbani kwaajili ya mapumziko mafupi.

“Mnapomaliza mitihani na kurudi nyumbani kunawatu wengi watawatazama na wengine wanaweza kujaribu kuwashawishi ili mjiunge nao hakikisheni mnawaepuka kwani watasababisha mshindwe kutimiza malengo yenu, “ alisema

“Simamieni na myaendeleze maadili mliyopatiwa na wazazi pamoja na walimu wenu hapa shuleni bado mnasafari ndefu ya kimasomo msije mkabweteka,” alisema.

Pia  amewataka kutumia elimu waliyoipata kupambana na changamoto za maisha kwani kunachangamoto nyingi  na aliwataka wasikubali kukatishwa tama na wakashindwa kutimiza malengo yao.

Mkurugenzi wa shule za St Mary's Mutta Rwakatale akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo  wanaomaliza darasa la saba  kwenye mahafali yaliyofanyika shuleni hapo. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo,  Jacob Mwangi
Mkurugenzi wa shule za St Mary's Mutta Rwakatale akifurahia jambo na wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo upande wa Mbagala wakati wa mahafali  yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki
Wanafunzi  wa shule ya St Mary's Mbagala wakionyesha umahiri  wa kucheza nyimbo mbalimbali kwenye mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika Jumamosi shuleni hapo
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...