Nteghenjwa Hosseah, Kahama
Wahenga
husema usiibe kabla Jua halijazama,pengine ndio kauli inayofaa kusemwa
kwa Wananchi wa Kata ya Kinaga iliyopo pembezoni mwa Halmashauri ya
Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Katikati
ya kukata tamaa kusikoelezeka kwa wananchi wa Kata ya Kinaga wanaofikia
idadi ya Elfu kumi na sita (16,000)kwa mujibu wa Taarifa za Manispaa ya
Kahama,Uzinduzi wa Nyumba sita za Walimu uliofanywa na Waziri wa
Tamisemi Ummy Mwalimu unaleta Ahueni ya kipekee kwao.
“Hongereni
sana kwa Juhudi za kujenga kuboresha Miundombinu ya Kusomea watoto wetu
mnazofanya ni Matumaini yangu kuwa Nyumba hizi tunazozindua leo
kwaajili ya Walimu wetu zitachochea Ufaulu wa watoto wetu kwakuwa sasa
Walimu watafundisha pasipo adha ya kuwaza Makazi”Amesema Ummy Mwalimu
Waziri wa Tamisemi.
Baadae Waziri Ummy
akamuagiza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dk. Grace Maghembe Kuingiza Kata
ya Kinaga kwenye orodha ya Kata za Kimkakati ili iweze kupatiwa fedha
za Ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachosaidia Akinamama Wajawazito
kujifungua salama pasipo vikwazo.
Pamoja na
Ahueni ya Kujengewa kituo cha Afya lakini pia Waziri Ummy amemuelekeza
Katibu Mkuu Tamisemi,Prof. Rizik Shemdoe kuwaagiza Tarura kuijenga
barabara ya Magobeko kwakiwango cha Changarawe ili iweze kupitika wakati
wote.
Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Dk. Philmon Sengati amesema Mkoa huo utendelea kutekeleza mipango
mbalimbali ya Kimaendeleo ikiwemo kusogeza karibu Huduma za Afya na
kuboresha Miundombinu ya Barabara.
Kata ya
Kinaga Katika Manispaa ya Kahama ndio kata iliyopo pembezoni kuliko
ikiwa na umbali wa Km 22 kutoka Makao Makuu ya Halmashauro ya Kahama.Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu akifungua nyumba za Walimu
(6 in 1) zilizojengwa katika Shule ya Msingi Magobeko Kata ta Kinaga
kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Philemon Sengati
Waziri wa Nchi OR- TAMISeMI Mhe. Ummy Mwalimu akitoa pongezi kwa Uongozi
wa Manispaa ya Kahama baada ya akifungua nyumba za Walimu (6 in 1)
zilizojengwa katika Shule ya Msingi Magobeko Kata ta Kinaga kwenye
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na hadhara
wakati wa hafla ya kufungua nyumba za Walimu (6 in 1) zilizojengwa
katika Shule ya Msingi Magobeko Kata ta Kinaga kwenye Halmashauri ya
Manispaa ya Kahama.
Muonekano wa Nyumba za Walimu ( 6 in 1) zilizofunguliwa na Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake kwenye Manispaa ya Kahama.
Muonekano wa Nyumba za Walimu ( 6 in 1) zilizofunguliwa na Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake kwenye Manispaa ya Kahama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...