ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusibilo  Mwakabibi na Mwenzake  Eduward   haule wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya utumishi.

 Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi Ester Martin aliyekuwa akisaidiana na wakili wa serikali Mwandamizi Mkunde Mshanga  mbele Ya hakimu mkazi mwandamizi Evodia Kyaruzi imedai washtakiwa wametenda kosa hilo kati ya Machi  2020 na Machi 2021 katika Mkoa wa Dar  es Salaam.

 Katika shtaka la matumizi mabaya ya madaraka imedaiwa, katika kipindi hicho, mshtakiwa Mwakabibi akiwa ameajiriwa Kama Mkurugenzi na Mratibu wa mradi wa DMDP walitekeleza  ujenzi  wa kituo cha basi cha Buza katika Kiwanja Kilichopo  buza kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana bila ruhusa.

 Katika shtaka la Matumizi mabaya ya  ofisi  inadaiwa washtakiwa hao wakiwa waajiriwa wa Manispaa Ya Temeke Kama Mkurugenzi na Mratibu wa  Mradi wa DMDP  kwa maksudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kwenda kinyume na sheria ya Ardhi.

 Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu kwa kuwa shtaka linalowakabili ni la uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na upande wa utetezi umeiomba mahakama itumie kifungu cha 29 (4) cha sheria ya Uhujumu Uchumi Ili kuwapa dhamana washtakiwa kwa kuwa mashtaka waliyosomewa  hayajataja Kiwango cha chochote cha fedha.

 Pia wameiomba Mahakama  kuweka  masharti nafuu ya dhamana yatakayowasiadia washtakiwa kufika mahakamani kila terehe itakayopangwa.

 Hata hivyo, upande wa mashataka umedai kuwa hauna pingamizi ya dhamana 

 Akisoma masharti ya dhamana washtakiwa wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh. milioni Kumi  ama hati ya mali  isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa. Pia washtakiwa wametakiwa kutotoka nje ya nchi bila Kibali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 2, 2021 ambapo Itakuja kwa ajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...