Na Mwamvua Mwinyi,Kibiti
Wanawake
wa eneo la Bungu ,Wilayani Kibiti wanatarajia kuondokana na changamoto
kubwa ya ufinyu wa chumba cha kujifungulia waliyoipata kwa zaidi ya
miaka 25 iliyopita baada ya kukamilika kwa jengo la wodi ya wazazi na
choo zahanati ya Bungu.
Wanawake
hao kipindi hicho walitaabika kuzaa kwa mbanano na wengine kuzalia
chini ,kutokana na ufinyu wa chumba na upungufu wa vitanda ambapo
vilikuwa vitanda viwili .
Pamoja
na hayo ,kulikuwa na kero ya maji iliyosababisha mjamzito kwenda
kujifungua na maji kutoka nyumbani na vibatari kwa kukosekana nishati ya
umeme.
Akizindua jengo
la wodi ya wazazi na choo katika zahanati ya Bungu , kiongozi wa mbio
maalum za mwenge wa uhuru ,LT.Josephine Mwambashi alisema , serikali
inajitahidi kuhakikisha inaondoa matatizo ya upungufu wa majengo ya
uzazi na upasuaji.
Alisema , serikali pia inapambana kutatua changamoto mbalimbali za afya ikiwemo vifaa tiba ,dawa na majengo mbalimbali.
Akitoa
taarifa ya mradi mganga mfawidhi zahanati ya Bungu,Luhalala Jackson
alielezea,umegharimu milioni 40 ,387,457 zikiwa ni fedha kupitia mradi
wa malipo kwa ufanisi (RBF).
"Mradi
huu una faida kubwa kwa wananchi wa Bungu na maeneo jirani hususan
akinamama wajawazito wanaofika kituoni kwa ajili ya huduma za uzazi "
Luhalala
alifafanua ,lengo ni kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto
wachanga kwa kuhakikisha wanapata huduma bora na kwa wakati .
Alibainisha
,wastani zahanati hiyo inahudumia wagonjwa 16,292 (OPD) ambapo wanaume
ni 7,210 na wanawake 9,082 kwa mwaka ,kwa wiki wanajifungua kina mama 15
sawa na wateja 60 kwa mwezi ,ambapo kwa mwaka mzima ni wateja 400 hadi
720.
Mkazi wa Bungu
,Amina Mnjopeka alisema ,wanaishukuru serikali kwa kusogezewa huduma
hiyo kwani miaka zaidi ya 20 walitaabika hasa katika tatizo la chumba
kidogo cha kuzalia,maji na umeme.
Mwenge wa uhuru umepokelewa Kibiti agost 15 ukitokea Rufiji na agost 16 Jumatatu utapokelewa Wilayani Mkuranga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...