Na Amiri Kilagalila,Njombe
Ikiwa
ni siku chache tangu waziri wa Nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na
serikali za mitaa Ummy Mwalimu kuagiza kuanza mara moja ujenzi wa ofisi
za halmashauri ya wilaya ya Njombe.Timu ya wataalamu kutoka halmashauri
hiyo iliyoambatana na mkurugenzi imetembelea na kukagua maeneo makubwa
matatu ya halmashauri iliyokabidhiwa na wananchi wa kijiji cha
Kidegembye bure ili kuanza ujenzi.
Akitoa
taarifa ya vipimo ya eneo mojawapo mara baada ya timu hiyo
kukagua,Afisa wa mipango miji wilaya ya Njombe Erick Chigome amesema
eneo mojawapo mara baada ya kufanyiwa vipimo limebainika kuwa na ukubwa
wa ekari 75 na kuwa na utosherevu wa ujenzi wa taasisi za serikali
takribani 20
“Kwa ujumla
tulivyofika na kulipima eneo hili limetoa ekari 75 na kwasababu hiyo
tunakusudia kuwa na taasisi takribani 20 na wananchi wameridhia eneo
hili na kutoa eneo hili kwa ajili ya ujenzi wa halmashauri”alieleza
Chigome
Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya hiyo Valentino Hongoli amewashukuru wananchi kwa
kutoa eneo hilo kubwa bila ya kuwa na fidia yeyote na kuwaagiza
wataalamu kuja na ushauri mzuri juu ya ujenzi katika maeneo hayo
likiwemo eneo lingine la ekari 10 la karibu ndani ya kijiji hicho ambalo
tayari lilishapatikana BOQ.
“Haya
ni maeneo yetu lakini wataalamu mtushauri ipasavyo na waziri alishatupa
ushauri,na kama ninyi wataalamu mnaona kwamba hakuta kuwa na mtikisiko
wowote wa bajeti basi tunaweza tukaja hapa kwenye ekari 75 badala ya
pale kwenye ekari 20.Mfano pale tumetumia milioni 48 za kupimia tu kwa
hiyo tunawategemea wataaalamu kuona tunafanyaje”alisema Hongoli
Aidha
amesema kwa kuwa eneo la karibu lenye ekari 10 tayari limeshapimwa na
BOQ imepatikana wanategemea kuanza moja kwa moja ili kupunguza muda wa
ujenzi na hatua za upimaji katika eneo hilo jingine lenye ekari 75.
“Pale
kwenye ekari 10 pameshapimwa tayari kilichobakia ni utekelezaji tu
tungeenda haraka lakini pia bara bara ya Lami inapita kule kwa hiyo
tukijenga hapa mwananchi atalazimika pia kuongeza ghalama,sisemi hivi
ili kubatilisha mawazo ya wataalamu kama mna ona hatutaathiri bajeti
wala hatutachelewa tunawasikiliza ninyi”aliongeza Hongoli
Kwa
upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi,Sharifa
Yusuph Nabarang’anya amesema wanatamani kuona taasisi zinapatikana
katika eneo moja ili kuwasaidia wananchi kupata huduma kwa haraka huku
akishukuru wananchi wa kijiji hicho kwa kutoa eneo tayari kwa kuanza
ujenzi.
“Tumelipokea eneo
hili na tuko tayari kuanza taratibu nyingine za ujenzi na kabla ya
ujenzi tutatoa taarifa katika maeneo haya mawili ni wapi tutaenda
kujenga”alisema Bi,Sharifa Yusuph Nabarang’anya
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya hiyo Bi,Sharifa Yusuph Nabarang’anya
aliyeongozana na wataalamu ametembelea na kuyapokea maeneo yote matatu
moja lenye ekari 75 na lenye ekari 10 huku moja likiwa bado
halijabainika ukubwa wake na maeneo yote yakiwa yanapatikana katika
kitongoji cha Ikombe kijiji cha Kidegembye.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi,Sharifa Yusuph
Nabarang’anya akizungumza mara baada ya kukagua na kupokea eneo la
ujenzi wa ofisi za halmashauri na kuahidi kuanza ujenzi mara moja.Baadhi ya wataalamu wakimuonyesha mkurugenzi mwisho wa
eneo la halmashauri hiyo walilokabidhiwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi
wa ofisi za halmashauri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...