Na Amiri Kilagalila
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe (UWT)
Scolastika Kevela ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Yono
Auction Mart amewataka wakurugenzi wapya walioteuliwa kwenda kuchapa
kazi kwa juhudi ili kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza
mkoani Dar es Salaam,Mama Kevela alisema ni vyema wateuliwa hao wapya
wakatambua kuwa wameaminika hadi kupewa nafasi hizo hivyo hakuna sababu
yoyote ya wao kwenda kuleta uzembe katika utekelezaji wa majukumu yao
na kwamba kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuangusha Rais Samia
aliyewateua.
“Rais
ametimiza wajibu wake kikatiba wa kuwateua hivyo ni vyema waende
wakachape kazi kwa weledi ili kumsaidia katika majukumu mbalimbali ya
ujenzi wa Taifa na kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika maeneo
waliyopangiwa”amesema Mama Kevela
Rais
Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa wiki alifanya uteuzi wa wakurugenzi
184 wakiwemo wapya 69 ambapo kati yake wanawake ni 33 sawa na asilimia
48 huku katika idadi ya jumla ya wakurugenzi wote 184 wanawake wakiwa
55 sawa na asilimia 29.
Akilizungumzia
hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI)Ummy Mwalimu mbali na kumshukuru Rais Samia kwa kuteua
wanawake nusu ya idadi ya wakurugenzi wapya, alisema hatua hiyo ni kubwa
kwa wanawake na kwamba Rais anastahili pongezi.
“Tunamshukuru
Rais Samia kwa kuendelea kupigania usawa katika nafasi mbalimbali za
uongozi hapa nchini, idadi hii ya wakurugenzi wapya aliowatua inazidi
kutupa motisha na chachu ya kuongeza bidii katika kazi sisi kama
wanawake, kikubwa tuendelee kuchapa kazi ili kumsaidia katika utendaji
wake” alisema Ummy
Aidha
akilizungumzia hilo Mama Kevela alisema yeye kama Mwenyekiti wa UWT Mkoa
wa Njombe uteuzi wa idadi ya wanawake 33 katika nafasi hiyo ya
ukurugenzi imemfurahisha kwa kuwa inazidi kuondoa pengo la uwiano kati
ya wanawake na wanaume huku akiwataka wanawake hao kwenda kuchapa kazi
ili kumtia moyo Rais Samia.
Alisema
Rais Samia amewaamini kwa kiasi kikubwa hadi kuwachagua katika nafasi
hizo na kuwaacha wengine wengi waliopo na kwamba kwa sasa jukumu lao
kubwa ni kwenda kumuwakilisha katika nafasi walizopewa ili
kuudhihirishia umma kuwa walistahili katika nafasi hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...