Mkuu waMKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makala amezindua Kampeni ya usajili kwa walipakodi wapya ikiwa ni utekelezaji wa wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutanua wigo wa ukusanyaji  Kodi kwa watu wote.

Pia amewataka wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanasajili biashara zao na kulipa kodi kwa wakati ili wasiwe sehemu ya watu wanaovunja sheria.

Makala, ameyasema hayo leo Agosti 5, 2021 wakati akifungua kampeni za uandikishaji wafanyabiashara wapya unaofanywa na Mamlala ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanyika katika soko la Makumbusho, Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makala amesema uandikishwaji wa walipa kodi utasaidia jiji kutokuwa na wa wafanyabiashara wa wanaovunja sheria.

Amesema kodi ni jukumu kuu la kisheria hivyo kama  mfanyabiashara halipi kodi basi anakuwa amevunja sheria, hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara ambao bado hawajasajili biashara zao kuzisajili ili waweze kutambulika na kutimiza matakwa ya kisheria la ulipaji wa Kodi.

Aidha Makala amewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu zao ili kurahisisha Zoezi la ukadiriaji na ukusanyaji wa Kodi huku pia akiwasisitiza kutoa risiti wanapouza bidhaa zao na amewataka wananchi kudai risiti pindi tu wakinunua kitu.

RC Makala pia ameipongeza TRA Kwa Mapinduzi makubwa Katika ukusanyaji wa kodi jambo lililowezesha kupanda kwa Mapato na kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Aidha RC Makala amewataka baadhi wafanyabiashara wakubwa  kuwatumia wamachinga ili kukwepa kodi na kuikosesha serikali mapato kuacha kufanya hivyo mara moja.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema mbali na usajili huo pia watakuwa wakitoa bure namba ya utambulisho kwa mlipa kodi pamoja na Tax Clearance ili kuhakikisha wote wanaofanya biashara wanasajiliwa.

"Tunathamini sana mchango wafanyabiashara ambao  amekwishasajiliwa na wanalipa kodi, kwani ulipaji kodi wao umekuwa chachu kuu ya maendeleo ya Taifa letu", amesema Kidata.

"Kwa sasa nchi yetu imeweka kipaumbele katika kuhakikisha mapato ya serikali yanakusanywa kwa ufanisi, kwa kuzingatia umuhimu huo napenda kuwakumbusha wajibu wetu kama wafanyabiashara na wananchi kuhakikisha umesajili na kuandikishwa kama mlipakodi ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu" amesema Kidata.

Pia amewasisitiza wafanyabiashara kutunza kumbukumbu   kwani utunzaji wa kumbukumbu ni suala muhimu katika ukadiriaji na ukusanyaji wa kodi. " Ni muhimu wafanyabiashara wote tutunze kumbukumbu ili kuwezesha maofisa wetu kukadiria kodi stahiki kwani serikali haitaki kabisa kukusanya kodi zisizo na msingi".

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara namba ya usajili wa biashara wakati wa kampeni ya usajili wa walipakodi  wapya wa Mkoa wa Dar es Salaam. Ufunguzi wa kampeni hiyo  umefanyika leo Agosti 5,2021 katika soko la Makumbusho Mkoani Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni za uandikishaji wafanyabiashara wapya wa Mkoa wa Dar es Salaam. Ufunguzi huo umefanyika leo Agosti 5,2021 katika soko la Makumbusho Mkoani Dar es Salaam.

Wadau mbali mbali kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) na wafanyabiashara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala  wakati wa ufunguzi wa kampeni za uandikishaji wafanyabiashara wapya wa Mkoa wa Dar es Salaam. Uliofanyika katika soko la Makumbusho Mkoani Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi  kutoka  TRA Richard Kayombo akizungumza katika ufunguzi huo
Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani  TRA, Herbert Kabyemela akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni ya usajili wa walipakodi  wapya wa Mkoa wa Dar es Salaam. Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 5,2021 katika soko la Makumbusho Mkoani Dar es Salaam.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...