Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi vifaa vya kunawia mikono kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wikaya ya Tu duru, Hairu Hemedi Musa kwaajili ya baadhi ya Shule ya Sekondari ziliyopo Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia moja ya mashine ya kubangua korosho inayotumiwa na vikundi cha Wanawake Wajasirimali Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikata utepe kuzindua mashine za kubangua korosho zilizotolewa na Shirika la Viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Ruvuma kwa vikundi cha Wanawake Wajasirimali.



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia bidhaa za wanawake wajasirimali katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

……………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu, Tunduru

Serikalii imesema haitofumbia macho Shirika lolote Lisilo la Kiserikali litakalofanya kazi kinyume na Katiba zao na dhumuni la Shirika husika.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis alipofanya ziara katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma kukagua shughuli mbalimbali za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Wilayani humo.

Naibu Waziri Mwanaidi amesisitiza kuwa lengo la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni kusaidia pale ambapo Serikali haijafika katika kutoa huduma kwa jamii na sio vinginevyo.

“NGOs hizi zinasajiliwa kwa mujibu wa Sheria sasa niziombe tu zifanye kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo hatutofumbia macho ukiukwaji wowote wa Sheria na taratibu” alisema Mhe. Mwanaidi

Aidha ameongeza kuwa zipo changamoto nyingi katika jamii ikiwepo vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikikatisha ndoto za watoto wa kike walio wengi katika meneno mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tunduru ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Dkt. Julius Kenneth Ningu amesema watahakikisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi katika Wilaya ya Tunduru na Mkoa kwa ujumla yanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.

“Tutahakikisha NGOs zinafuata Sheria na zinafanya kazi kwa mujibu wa usajili wao na kuwanufaisha wananchi” alisema Dkt. Ningu

Ameongeza kuwa Wilaya itasimama vizuri katika kuhakikisha inawachukulia hatua wanaosababisha kuwepo kwa mimba za utotoni

Akizungumza Mratibu wa Mradi wa Afya Mama na Mtoto Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Masasi Phares Lihewe amesema mradi huo umechangia katika kutoa elimu na vifaa vya kunawa mikono ikiwa ni hatua za kujikinga na UVIKO 19 katika Shule mbalimbali za Sekondari Wilayni Tunduru.

Katika ziara yake Wilayani Tunduru Naibu Waziri Mwanaidi amekabidhi vifaa vya kunawa mikono kwa baadhi ya Shule za Sekondari Wilayani humo na kukagua shughuli za kiuchumi za wanawake wajasirimali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...