WAZIRI wa Maji Mh. Jumaa Aweso ametembelea na kukagua Mradi wa Maji Njedengwa jijini Dodoma, akiwa katika eneo la mradi amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bil.2.7 kwa ajili ya Utekelezaji wa Mradi huo.

Waziri Aweso ameagiza katika kipindi cha miezi miwili mradi ukamilike na wananchi wapate Maji.
Mradi huu utahudumia eneo la Njedengwa, Iyumbu, Soko la Ndugai, Stendi mpya,Nyumba 300(Mwangaza), eneo la FFU na Nzuguni pamoja na kuongeza kasi ya upatikanaji wa Maji maeneo mengine ya Jiji la Dodoma.

Aidha amemteua msimamizi wa mradi huo na miradi ya kimkakati ya Maji jijini Dodoma Mhandisi Kashilimu Mayunga Meneja Ufundi Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na atapangiwa kituo cha kazi.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...