Na.Khadija Seif, Michuzi Tv


MJUMBE mpya wa Kamati ya uchumi katika chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoani Kagera ahaidi kuhamasisha kutoa Elimu ya ulipaji kodi kwa Wananchi na jinsi gani ataweza kubadilisha fikra ya wananchi kuhusu tozo mbalimbali kama ni kitendo cha unyonywaji.


Akizungumza na Michuzi Tv Mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mjumbe wa Kamati ya uchumi wa chama hicho Regina Samwel zachwa amesema atatumia vizuri cheo hicho na kuhakikisha Maendeleo katika Mkoa wa Kagera kwa kupitia ukusanywaji wa Kodi na kuhakikisha serikali inaongeza Somo la ziada ya kutoa elimu ya kulipa Kodi Mashuleni ili iwe rahisi zaidi kuwa na Mazoea ya  kulipa kodi.


"Bado Kuna changamoto Sana kuhusu ulipaji kodi  na nchi yoyote ile iliyoendelea lazima kuwepo na ukusanywaji mzuri wa kodi ili fedha zinazopatika ziende kutengeneza miradi mbalimbali katika jamii na hata nchi kwa ujumla hivyo basi nitahakikisha wanafunzi wanapata Somo la ulipaji kodi ili waanze kupenda na kujenga Mazoea pia kisiwe kitu kigeni kwao kama ilivyo kwa Sasa kwa baadhi ya Wananchi."


Zachwa ameomba Ushirikiano kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera katika kila hatua ambayo inalenga Kuboresha Sekta ya uchumi na kushikana bega kwa bega ili kuleta Mabadiliko na Maendeleo mkoani humo.


"Sio Mgeni na Maswala ya kodi hivyo ni sehemu ama cheo ambacho nitakifanyia kazi inavotakikana  kutokana na nimesomea maswala ya kodi chuo cha udom."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...