Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) leo imezindua ripoti inayoelezea uwekezaji wake kwa jamii. Ripoti hiyo ya mwaka 2020, inaelezea kwa undani uwekezaji ambao kampuni hiyo imeufanya kwa jamii katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania ambako inafanya biashara zake.

Kwa Tanzania miradi ya uwekezaji kwa jamii inatekelezwa na kampuni tanzu ya EABL, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama, programu ya kilimo biashara inayowasaidia wakulima wazawa, unywaji wa kistarabu, programu za ujumuifu pamoja na utunzaji wa mazingira kupitia kupanda miti. Miradi hiyo inatekelezwa chini ya mpango wa kusaidia jamii unakwenda mpaka 2030.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, mkurugenzi mtendaji wa SBL Mark Ocitti alielezea baadhi ya miradi inayotekelezwa na kampuni hiyo akianza na miradi ya kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama ambapo alisema SBL imeweza kuwafikishia huduma hiyo muhimu Watanzania milioni mbili ikilenga kurudisha kila tone inalotumia katika uzalishaji wa bidhaa zake. SBL imetekeleza miradi 21 ya maji hapa nchini tangu mwaka 2010.

“Mwaka 2020 tumenunua tani 17,000 za nafaka sawa na asilimia 70 ya mahitaji yetu ya malighafi tunazotumia katika uzalishaji wa bidhaa zetu kwa mwaka ikiwa ni pamoja na shayiri, mahindi na mtama. Katika programu hii inayojulikana kama kilimo biashara, tunafanya kazi na wakulima zaidi ya 400 katika mikoa nane tukiwasaidia kwa kuwapa mafunzo ya kilimo endelevu, huduma za ughani pamoja na kuwaunganisha na taasisi za fedha kwa ajili ya kupata mikopo ya kuongeza uzalishaji wao,”

Mradi mwingine ni pamoja na programu ya kusaidia kuongeza wataalamu wa kilimo kupitia kutoa ufadhili wa masomo maarufu kama Kilimo Viwanda ambayo tayari imeshawanufaisha wanafunzi 70 wanasomea masomo ya kilimo katika vyuo vinne vya kilimo hapa nchini.

Elimu juu ya unywaji wa kistarabu ni mradi mwingine ambao umekuwa ukitekelezwa na SBL . Mradi huu umeweza kuwafikia maelfu ya Watanzania kupitia kampeni yake ya ‘Usinywe na Kuendesha chombo cha Moto’. Kampeni hii inawalenga madereva wa vyombo vya usafiri vya umma, waendesha boda boda, waenda kwa miguu, wanafunzi wa vyuo na makundi mengine.

Uzinduzi wa ripoti hiyo ulienda sambamba na mjadala juu ya kujenga sekta imara na endelevu ya kilimo ambao uliwaleta pamoja wataalamu kutoka nyanja mbali mbali. Waliohudhuria ni pamoja na mamlaka za udhibiti, wavumbuzi, wafanya biashara, wakulima, wafanya maamuzi, wachumi na wanadiplomasia




Washiriki wa mjadala wa namna ya kuboresha kilimo wakizungumza muda mfupi baada ya uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji kwa jamii wa kampuni ya EABL ambayo inamiliki Kampuni ya Bia ya Serengeti. Kutoka kushoto ni Geoffrey Kirenga afisa mtendaji mkuu wa SAGCOT, Prof Honest Ngowi kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Dar es Salaam, Audax Rukonge mkurugenzi mtendaji wa ANSAF, Rose Funja, Mkugenzi mtendaji wa Agrinfo na Maximillian Sarakikya makamu mkuu wa chuo cha Kilimo Kaole Bagamoyo.


Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya SBL John Ulanga (wa pili kulia) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT Geoffrey Kirenga ( wa tatu kulia) muda mfupi baada ya uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji kwa jamii ya SBL (Sustainability Report). Kulia ni deputy British High Commissioner to Tanzania Rick Shearn na kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Serengeti Mark Ocitti
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) John Ulanga, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji kwa jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya uwekezaji kwa jamii wa kampuni hiyo uliyofanyika wajijini Dar es Salaam jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...