Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo kulia akitiliana saini ya makubaliano
na Mhandisi wa Uzalishaji na Mauzo kutoka Kampuni ya Kahama Oils Mills Limited Alfred
Shima kushoto
kwa ajili ya usambazaji wa mabomba yenye thamani ya Milioni 419 kwa ajili ya
kuhudumia miradi minne katika vijiji vinne vilivyopo kwenye wilaya za
Handeni,Mkinga,Kilindi na Lushoto kulia ni Meneja wa Ruwasa
wilaya ya Mkinga Mhandisi Kaijage Thomas Mzee na wengine ni watumishi wa Ruwasa mkoa wa Tanga.

Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo katikati akionyesha
waandishi wa habari makubaliano hayo yaliyoingia na Mhandisi wa
Uzalishaji na Mauzo kutoka Kampuni ya Kahama Oils Mills Limited Alfred
Shima kushoto na kulia ni Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mkinga Mhandisi
Kaijage Thomas Mzee.
Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza na
waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika utiliaji wa saini
makubaliano hayo.
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
WAKALA wa Usambazaji wa Maji Safi
na Usafi wa Mazingira Vijijini ( Ruwasa} Mkoa wa Tanga leo wameingia makubaliano
na Kampuni ya Kahama Oil Mills Limited
kwa ajili ya usambazaji wa mabomba yenye thamani ya Milioni 419 kwa ajili ya
kuhudumia miradi minne katika vijiji vinne vilivyopo kwenye wilaya za
Handeni,Mkinga,Kilindi na Lushoto.
Halfa ya makubaliano hayo
ilifanyika leo kwenye ofisi za Ruwasa zilizopo eneo la Gofu Jijini Tanga ambapo
Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo aliingia makubaliano
hayo na Mhandisi wa Uzalishaji na Mauzo kutoka Kampuni ya Oil Kahama Alfred
Shima.
Akizungumza mara baada ya
makubaliano hayo Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo alisema
miradi hiyo ni upanuzi wa mradi wa maji eneo la Mkata wilayani Handeni,Ujenzi
wa mradi mpya wa Mahezangulu wilaya ya Lushoto,Ukarabati mkubwa wa mradi wa
Maji Maraba wilaya ya Mkinga na Mradi wa Maji Mafisa wilaya ya Kilindi.
Alisema miradi hiyo itakapokamilika
itaongeza idadi ya watu 28,638 katika upatikanaji wa huduma watu hao ni sawa na
asilimi 1 ya watu wa Tanga watakuwa wamepata hduuma ya maji safi na salama.
Mhandisi Lugongo alimtaka msambazaji
wa mabomba hayo kuhakikisha anayasambaza mapema na ndani ya mwezi mmoja baada
ya siku 14 kutoka leo mabombo yafike kwenye miradi ili kazi ziweze kufanyika na
wananchi waanza kupata huduma.
Awali akizungumza Meneja wa Ruwasa
wilaya ya Mkinga Mhandisi Kaijage Thomas Mzee aliwataka wananchi kwenye maeneo ambayo mabomba
hayo yanakwenda wahakikishe wanaitunza miundombinu hiyo ili lengo la mradi
liweze kufikiwa.
Naye kwa upande wake Mhandisi wa
Uzalishaji na Mauzo ya Kampuni ya Kahama
Mills Mhandisi Alfred Shima alihaidi wana Tanga kwamba watawapelekea mabombo
yenye ubora kwa ajili ya kusambaza katika miradi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...