Mkandarasi wa China railway seventh group anayejenga bara bara kipande cha Moronga Makete akimuonyesha naibu waziri wa ujenzi namna wanavyopasua miamba ili kufanikisha ujenzi wa barabara katika maeneo ya Makete.
Meneja wa Tanroad mkoa wa Njombe mhandisi Ruth Shalluah akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi katika kipande cha Moronga -Makete

Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi mhandisi Godfyrey Kasekenya akizungumza katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda alipofika kuonyesha uwepo wake katika wilaya hiyo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa bara bara ya Njombe –Makete kwa kiwango cha lami.


SERIKALI imetangaza tenda ya ujenzi wa bara bara kwa kiwango cha lami kutoka wilayani Makete mkoani Njombe kwenda Isyonje mkoani Mbeya kilomita 25 kwa kuanza huku ikiendelea kujipanga kukamilisha ujenzi wa kilomita 96.4 za bara bara yote ili kuweza kufungua mikoa miwili ya Njombe na Mbeya kupitia wilaya ya Makete.

Hayo yamebainishwa na naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi mhandisi Godfyrey Kasekenya (MB) wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa bara bara ya kutoka Njombe kuelekea wilayani Makete yenye urefu wa kilomita 107.4 kwa kiwango cha lami.

“Tumetangaza barabara yenye urefu wa KM 25 kwa kuanza kaunzia Makete kwenda Isyonje na kadri fedha itakavyopatikana lengo ni hii bara bara iweze kukamilika yote,kwa hiyo tutahakikisha inakamilika kwa haraka sana ili tuweze kupafungua hapa na watu waweze kusafirisha bidhaa zao”alisema mhandisi Godfyrey Kasekenya 

Licha ya kutangaza tenda hiyo Kasekenya amesema serikali imepokea changamoto mbali kutoka kwa mkandarasi pamoja meneja wa Tanroad mkoa wa Njombe ikiwemo kukosekana kwa siment hatua inayosababisha kuchelewa kukamilika kwa bara bara kipande cha Moronga-Makete kilometa 53.5 inayojengwa na mkandarasi China railway seventh group.

“Kama tunavyoelewa katika maeneo haya ya Makete kuna mvua nyingi hii imesababisha kupunguza kasi ya ujenzi pia kulikuwa na upungufu wa vifaa”alisema mhandisi Ruth Shalluah meneja wa TANROAD mkoa wa Njombe

Kasekenya amesema “Swala la siment ambalo tumepata taarifa kutoka kwa mhandisi ambao kutokana na upungufu kumefanya waweze kurudi nyuma kidogo nadhani swala hilo linashughulikiwa ili kazi isisimame na kuedelea kufanya kazi lakini tunashukuru kwa kazi inakwenda vizuri” 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda amesema kufunguliwa kwa bara bara ya Makete kwenda mkoani Mbeya kutaongeza kuimarika kwa uchumi wa wananchi wa Makete.

“Mkitusaidia barabara ile ikafunguka na mawasiliano ya kwenda Mbeya yakafunguka tunaamini uchumi wetu kwenye wilaya hii utafunguka sana na wananchi wetu watafurahia zaidi”alisema Juma Sweda

Baadhi ya wananchi wananchi akiwemo Salome Chaula na Karim Mhanje wameipongeza serikali ya awamu ya sita kuendelea kuonyesha matumaini ya kukamilisha bara bara hiyo kwa kuwa awali walionyesha kupoteza matumaini kutokana na kufarikia kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt,John Pombe Magufuli kwa kuwa bara bara hiyo ilianza kujengwa katika uongozi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...