Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU
wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema ,uongozi wa mkoa unatarajia
kuanza ziara ya kata kwa kata ,lengo likiwa ni kusikiliza kero ,na
kutembelea miradi ya kimkakati iliyopo mkoani hapo.
Aidha
mkuu huyo ,amedhamiria kuvalia njuga kero kubwa ya migogoro ya ardhi
ambapo baadhi imeshaanza kutatuliwa kupitia kampeni ya ondoa migogoro
ya ardhi kwa kushirikiana na Waziri wa ardhi.
Kunenge
aliyaeleza hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa
Pwani , kufahamiana na kujiwekea malengo ya mpango kazi Ili kuutangaza
Mkoa wa Pwani .
Alieleza
,hatua iliyopo sasa ni wataalam wa mkoa wapo katika maeneo mbalimbali
kisha itapangwa ratiba rasmi ya ziara hiyo ambapo wataambatana na jopo
la waandishi wa habari.
Hata
hivyo,alisisitiza ushirikiano na Waandishi wa habari na kuwaomba kuwa
wamoja ili kuutangaza mkoa huo ambao umesheheni viwanda,miradi mikakati
ikiwemo reli ya kisasa SGR,Mradi mkubwa wa umeme Rufiji-Stigo na vivutio
vya utalii .
"Bado
kuna gap ,mkoa haujatangazika ipasavyo, kuna viwanda vikubwa ,vivutio
vya utalii Saadan,Mafia lakini bado !!naomba tushirikiane watanzania
wajue yaliyomo ndani ya mkoa huu "alifafanua Kunenge.
Nae
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo ,alisema wataalamu
wapo katika wilaya mbalimbali wakimalizia kufanya tathmini
zilizoelekezwa ili kuanza ziara ya kata kwa kata.
Kwa
upande wake mwandishi wa habari kutoka nipashe Julieth Mkireri
,alishukuru kuwepo kwa mkutano huo na kusema unakwenda kuleta umoja na
kutimiza malengo ya mkoa.
Alieleza jukumu letu ni kuelimisha,kuhabarisha hivyo tutautangaza vema mkoa kama ilivyo kawaida ya majukumu yetu ya kikazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...