Na Amiri Kilagalila, Njombe


SHULE ya sekondari Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe inatarajiwa kujengwa jengo la ghorofa ili kuboresha miundombinu ya madarasa ya shule hiyo pamoja na kutumia vizuri eneo kutokana na udogo wa eneo la shule.


Mpango huo umebainishwa na diwani wa kata ya Uwemba Bwana Jactan Mtewele mara baada ya kutembelewa na mkuu wa wilaya ya Njombe aliyefika katika shule ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa mawili pamoja na kuzungumza na walimu.


“Wazo hili lilikuja sio tu kwa kuwa hakuna mazingira rafiki bali eneo limeisha kwahiyo tukaona ili kutumia eneo vizuri lilobaki tukapata wazo la kujenga ghorofa baada ya kuona miundombinu imechoka na eneo limekuwa finyu”alisema Mtewele


Kwa upande wake afisa elimu sekondari halmashauri ya mji wa Njombe Mwal,Prochesius Mguli amesema halmashauri imebariki mpango huo na kwamba halmashauri ipo tayari kuonyesha ushirikiano.


“Mpango huu aliuwasilisha kwenye idara yetu na sababu kubwa zipo mbili ikiwa eneo lake ni finyu kwa hiyo ikijengwa ghorofa eneo dogo litakuwa na madarasa mengi kwa hiyo sisi tulipokea na idara hii ilishiriki kuandaa BOQ kitaalamu kabisa na tumemkabidhi”alisema Mguli


Naye mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ametoa pongezi kwa diwani wa kata ya Uwemba kwa mpango huo huku akibainisha kuwa serikali ya wilaya ya Njombe itakuwa bega kwa bega katika ujenzi huo.


“Niendelee kuwaahidi mambo mazuri tutawaletea hapa na ujenzi wa ghorofa niseme tu tutaanza na tutafika hatua nzuri kwa kutumia kila njia ambayo tunaweza”alisema Gwakisa


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na diwani Mtewele amesema wanatarajia kuanza na ujenzi wa ghorofa moja itakayokuwa na madarasa manne.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...