DR. Alexander Mushi ambaye ni daktari bingwa wa watoto na muasisi wa 'Gaborone Childrens Care Clinic' amefariki dunia tarehe 18 Agosti 2021 huko Gaborone, Botswana alikokuwa akiishi kwa takribani miaka 30.
Mwili wa Marehemu Dr.Alexander Mushi umepokelewa jijini Dar es Salaam na taratibu za misa na kuaga mwili zitafanyika nyumbani kwa mtoto wake wa kiume Eng.Samwel Mushi maeneo ya Mbweni karibu na Bumera Lodge siku ya Jumanne tarehe 24 Agosti 2021 kuanzia saa tatu asubuhi.
Mazishi yatafanyika mkoani Kilimanjaro siku ya Alhamisi tarehe 26 Agosti 2021 nyumbani kwake Machame kuanzia saa saba mchana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...