Na.Khadija Seif , Michuzi Tv

Wenye mzio watakiwa kupata Ushauri kwa watoa huduma ya chanjo

BALOZI wa Nchini Marekani wa Tanzania amempongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona ipo haja ya wananchi kupata chanjo ya uviko 19 ili kupunguza Kasi ya vifo .

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kufungua programu ya Maswali na majibu kuhusu chanjo ya johnson & Johnson kwa wataalam wa tiba na afya kutoka ubalozi wa Marekani Donald wright amesema kumekuwepo na maswali mengi kwa wananchi juu ya umuhimu wa chanjo hiyo ya uviko 19 ambapo mwishoni mwa Julai 24 Mwaka huu Rais Mama Samia alipokea Msaada wa dozi milioni moja za chanjo dhidi ya uviko 19 aina ya Johnson na Johnson kutoka nchi ya Marekani.

"Mnamo Julai 28 nchi ya Tanzania ilizindua Kampeni ya kitaifa ya chanjo na Rais Samia Suluhu aliongoza Watanzania kwa kupata chanjo hiyo akiwa wa kwanza,hivyo nampongeza kwa uongozi wake katika suala hili na kufanya maamuzi thabiti ya kulinda afya za wananchi".

Hata hivyo wright amesema Marekani imedhamiria kwa dhati kuongoza mapambano ya dunia dhidi ya janga la uviko 19 na kuongeza Kasi ya usambazaji wa chanjo duniani.

"Tunafahamu kuwa hakuna aliye salama na kwa sababu hiyo utawala wa Rais wa Marekani  Biden unakusudia  kutoa dozi milioni 500 za chanjo kupitia mpango uitwao gavi kwa ajili ya kusambazwa katika ncchi 92 zenye uchumi wa chini na ule wa kati kupitia mpango wa covax na umoja wa Afrika  ili kuongeza nguvu  ya Mapambo ya kimataifa dhidi ya janga ya Hilo."

Aidha wright ameongezea kuwa Kutokana na kuwepo kwa janga hili la uviko 19 ambalo lineshasababisha vifo vingi na linaendelea kusababisha vifo zaidi ya milioni 4 duniani kote natoa shukrani kwa jitihada za kishujaa za wanasayansi wanaofanya kazi pamoja duniani kote,tuna nyenzo ya kulitokomeza janga hili na nyenzo hiyo ni chanjo dhidi ya virusi vya korona. 

Pia ameeleza kuwa pamoja na kwamba ushahidi upo wazi kutoka na vifo vinavoendelea bado watu Wana wasiswasi kuhusu chanjo dhidi ya virusi vya korona au kutopata taarifa za kutosha kuweza kufanya maamuzi.

"lakini maamuzi ya kimatabibu ni Miongoni mwa maamuzi muhimu kabisa tunayoyafanya maishani na ni muhimu kuwa na taarifa nyingi kwa kadri inavyowezekana."

Kwa upande wa Mtaalam kutoka ubalozi wa Marekani ambae ni daktari katika kitengo cha                Arkan ibwe amefafanua zaidi makundi ambayo yanatakiwa kutoa maelezo kwa mtoa huduma wa chanjo hiyo kabla ya kuchomwa chanjo hiyo ya Johnson na Johnson.

"Chanjo hiyo ni salama na ipo kwa ajili ya kusisimua Kinga ya mwili ili kutoweza kupata maambukizi au kupunguza Kasi ya ugonjwa wa uviko 19 na miongoni mwa watu ambao wanatakiwa kutoa taarifa zao kwa wahudumu haraka kabla ya kupata chanjo hiyo ni watu wenye mzio, presha pamoja na kisukari ili waweze kupatiwa msaada zaidi na kupatiwa Ushauri jinsi ya kupata chanjo hiyo."


Hata hivyo ibwe ameongeza kuwa Kuna weza kukajitokeza kwa baadhi ya maudhi madogo madogo pindi mtu apatapo chanjo hiyo kama vile kuvimba Mkono,kupata kichefuchefu,kulala,kuchoka mwili.

"Hali kama hiyo ni kiashiria tosha kuwa chanjo hiyo imefanya kazi hata hivyo  kupata chanjo sio mwisho wa kutokuepuka ugonjwa wa uviko 19 hivyo ningeshauri tuendelee kujikinga zaidi."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...