Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

UPANDE wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iuelekeze upande wa Jamuhuri kuhakikisha wanaleta maelezo ya mashahidi ili washtakiwa wajue hatma yao.

Hatua hiyo imefikwa baada ya mshtakiwa Mbowe na wenzake kuunganishwa kwa kusomewa mashtaka yao  pamoja na Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius Hilla ambapo baada ya kumaliza kusoma akadai kuwa upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amewataka upande wa Jamuhuri kurejea mwenendo wa kesi wa Julai 26 ambayo Mbowe alisomewa mashtaka peke yake ambapo walidai upelelezi umekamilika.

Kutokana na hali hiyo Wakili Hilla akadai upelelezi umekamilika ila walisema haujakamilika kwa sababu jalada la kesi hiyo liko kwa DPP kwa ajili ya kuandaliwa maelezo ya mashaidi.

Akijibu hoja hiyo Wakili Kibatala ndipo akaiomba Mahakama wauelekeze upande wa Jamuhuri kuhakikisha mwenendo wa kesi hiyo unanyooka itakapopangiwa tarehe nyingine wajipange kuleta maelezo ya mashahidi ili washtakiwa wajue hatma yao.

Amedai, upande wa mshtaka wanaiudisha kesi nyuma na kisheria siyo sawa. "Tunawasikia wapelelezi wakiuarufu umma kuwa upelelezi umekamilika na wanaenda mbali na kusema washtakiwa ametenda mambo ya ni hovyo hovyo, hivyo haya wanayoyasema leo ni kutuchanganya, na muhimu zaidi ni kuichafua mwenendo wa kesi," amesema Kibatala

Hakimu Simba akaeleza  ni vema mambo yafanyike haraka, hoja ya Kibatala inaweza kuwa na mashiko tujiweke vizuri.

Akijibu tena hoja hizo Hilla amedai, kwa ujumla upelelezi umeshafungwa kilichobaki ni DPP kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo unawakilishwa na mawakili wa serikali waandamizi Pius Hilla, Christopher Msigwa na Sylivia Mitanto huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na jopo la mawakili tisa wakiongozwa na  wakili wa utetezi Peter Kibatala, Jonathan Mndeme, John Malya na Frederick Kihwelo

Mbali na Mbowe washtakiwa wengine ni  Halfan Hassan, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.Washtakiwa wote wanakabiliwa na shtaka la kula njama ya kulipua vituo vya mafuta na mikusanyiko ya Umma.

Huku Mbowe peke yake akikabiliwa na shtaka la kufadhili vitendo vya kigaidi, na washtakiwa Hassan, Kasekwa Lingwenya wakidaiwa kupokea pesa kutoka kwa Mbowe kwa ajili ya kufanya vitendo vya kigaidi.

Pia mshtakiwa Kasweka anadaiwa kukutwa na silaha aina pisto na risasi tatu huku mshtakiwa Hassan akikutwa akitumia sare na vifaa vya jeshi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...