Na Amiri Kilagalila,Njombe


Viongozi wa dini nchini wameshauriwa kuacha kuwapotosha wananchi kuhusu chanjo ya Corona kwani kufanya hivyo ni kuiingilia serikali katika kutimiza majukumu yake kwa wananchi inaowasimamia.

Kauli hiyo imetolewa na Mwinjilisti Asifiwe Mwasanyamba wa Kanisa la Kiinjili na Kirutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini usharika wa Melinze mkoani Njombe wakati wa ibada ya kuliombea taifa kwa siku nane ili kuondokana na ugonjwa wa Uviko 19.

“Kuna wengine wanapotosha kwa kusema chanjo hii ni mbaya,niwaulize ni nani aliyechoma hapa Tanzania akaona ni mbaya? Niseme tu serikali imewajibika na ingekuwa ya ajabu kama isingeonyesha kuwajibika na niwaaambie wakati wa vita hatuchagui silaha kwa hiyo lazima silaha yoyote tuitumie”Alisema  Asifiwe Mwasanyamba 

Mwasanyamba ameongeza kuwa “Tusisikilize propaganda kwasababu wasemaji wa serikali tunao,hawa wakisema juu ya taifa tuwasikilize na kwa kuwa kuna wengine wanapotosha juu Chanjo hawa tuwapuuze.Kwa hiyo sisi kama wainjilisti tunasema hivi mtu akitaka Chanjo achanjwe na asipotaka asichanjwe” 

Kwa upande wake kiongozi wa usharika huo mchungaji Eliad Siwelwe amesema kanisa hilo limekuwa likiwatahadharisha waumini wake kunawa mikono na kuvaa barakoa wanapokuwa kwenye ibada na hata wakiwa kwenye shughuli zingine ili kuendelea kupambana na virusi vya Corona.

“Juu ya chanjo tunawahimiza watu waweze kuchanja kwasababu kila mtu na imani yake lakini pia tumekuwa tukiwahamasisha waumini kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata njia zote za kujikinga na corona” Eliad Siwelwe Mchungaji kiongozi Usharika wa Melinze

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo akiwemo Amina Ilomo na Osward Mng'ong'o wanasema tahadhari dhidi ya Uviko 19 wanachukua ingawa mpaka sasa baadhi yao hawajaamua juu ya kupokea chanjo ya Uviko 19 na kuendelea kusisitizana kila mmoja afaute nafsi yake,

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...