Na Humphrey Shao, Michuzi TV

Balozi wa India nchini Tanzania, Binnaya Srikanta Pradhan amefurahishwa na utendaji wa kituo cha Umahiri cha Tehama (ITCoEICT) cha Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kuongeza wadau wa sekta binafsi ambazo ni Huawei na Siemens na kuahidi kuendelea kukiimairisha kituo hicho kwa kuongeza nguvu ya mafunzo kwa wataalam wa DIT sambamba na kuongeza vifaa vya kisasa. 


Balozi Binnaya ameyasema hayo alipotembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)  kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya mradi wa kituo Cha umahiri Cha Tehema (ITCoEICT) kilichoanzishwa kwa ushirikiano baina ya India na Tanzania.
 
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam Profesa Preksedis Marco Ndomba  amesema kuwa Kituo kinatakiwa kuwawezesha wananchi kuhusu matumizi ya Tehama katika maeneo mbalimbali yakiwemo afya na mengineyo kupitia Tiba mitandao .

Prof. Ndomba amesema kwamba ili kufanikisha hilo, DIT inashirikiana na hospitali za Rufaa chini ya usimamizi wa Wizara ya afya.

Mkurugenzi wa Kituo cha umahiri cha Teknolojia ya Habari (TEHAMA) Dr. Kennedy Aliila alisema kituo hicho  kilianza rasmi 2009 na kuzinduliwa na aliyekuwa Rais  wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambapo mpaka sasa mradi umeweza kutoa mafunzo kwa zaidi ya walimu 500 kutoka mikoa ya Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam.


Aidha Aliila alisema kituo hicho kinasaidia masuala ya Utafiti kwa kusaidia Taasisi mbalimbali kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kusisitiza kwamba hicho ni kituo cha kitaifa na sio cha DIT pekee.

Dr. Aliila amesema kuwa mojawapo ya manufaa ya mradi huo ni mafunzo waliyotoa kwa watumishi wa taasisi kama TAMISEMI, Jeshi la Polisi pamoja na baadhi shule za msingi hapa nchini.

Balozi wa India nchini, Binaya Srikanta akitoa maelezo mara baada ya kusikiliza wasilisho la  Tasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Juu ya mradi wa Tehama ulioasisiwa baina ya Tanzania na India.
Mkuu wa chuo cha Teknolojia Dar es Salaam(DIT)  Prof. Preksedil  Ndomba,akizungumza wakati wa kumkaribisha balozi wa India nchini mara alipotembelea chuo hicho leo Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Tehama cha Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT),Dr.Kenedy Aliila akieleza taswira nzima ya kituo cha Tehama kichoaanzishwa baina ya Serikali ya Tanzania na India kwa lengo la kukuza Teknolojia nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Super Computer kilichopo katika Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam.,Dr.Nkundwe Moses Mwasaga akitoa maelezo kwa Balozi wa India nchini, Binaya Srikanta wakati wa ziara yake katika tasisi hiyo.
Mkuu wa chuo cha Teknolojia Dar es Salaam(DIT)  Prof. Preksedil  Ndomba akikabidhi Zawadi ya Kalenda kwa Balozi wa India  Binaya Srikanta
 Balozi wa India nchini ,Binaya Srikanta ,akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Tasisi ya Teknolojia  Dar es Salaam(DIT).
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...