KESI
ya tuhuma ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo( Chadema)Freeman Mbowe na wenzake watatu inatarajia kuanza
kusikilizwa Septemba 15, 2021 katika Mahakama Kuu kitengo cha makosa ya
Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mahakama ya Mafisadi.
Hatua
hiyo imekuja baada ya leoSeptemba 10, washtakiwa hao kusomewa maelezo
ya awali.Katika kesi hiyo upande wa mashtaka unatarajiwa kuita mashahidi
24 na vielelezo 19 ili kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa
huku upande wa utetezi ukitarajiwa kuwa ma mashahidi 11.
Mapema
akisoma maelezo ya awali,Wakili wa Serikali Tulumanywa Majigo amedai
mshtakiwa wa kwanza, wapili na watatu wote walikuwa waajiriwa wa Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walioudhulia mafunzo ya ukomandoo katika
kambi ya Ngerengere Mkoani Morogoro na waliofukuzwa kazi kutokana na
vitendo vya utovu wa nidhamu.
Majigo amedai kuwa washtakiwa hao
watatu wanafahamiana huku mshitakiwa wa nne (Mbowe) akiwa ni Mwenyekiti
wa Taifa wa chama cha siasa cha CHADEMA.
Wakili huyo amedai
washitakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama,
mshitakiwa wa kwanza na wapili wanashtakiwa na makosa ya kukutwa na mali
iliyokusudiwa kutumika kutenda vitendo vya kigaidi huku mshitakiwa wa
nne pekee akikabiliwa na shitaka la kutoa fedha kwa ajili ya kufadhilii
vitendo vya kigaidi.
Majigo amedai Kwamba Julai mwama 2020 mbowe Aliomba Kukutana na Luten Denis Urio ambaye walikuwa wanafahamiana awali.
Waliafikiana
kukutana na baadae walikutana katika moja ya mgahawa uliopo maeneo
ya mikocheni na wakiwa katika eneo hilo Mbowe alimuomba Luten amtafutie
Makomando waliofukuzwa kazi ili wamsaidie katika kutekeleza vitendo vya
kigaidi ambavyo ni kulipua vituo vya mafuta mikusanyiko ya umma katika
maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaama, Mwanza na Arusha.
Wakili
ameendelea kudai kuwa Mbowe alimweleza Luteni Hurio lengo la kutaka
kufanya hivyo ni kuleta taharuki kwa wananchi na kuharibu misingi
iliyopo nchini kisiasa na kiuchumi.
Imeendelea kudaiwa kwamba,
Mbowe alitoa Sh Laki 699,000 ili kuwezesha makomando aliotafutiwa ambao
kwa sasa ni washtakiwa wenzake kuja Dar es Salaam ili kupanga namna ya
kutekeleza ugaidi huo.
Inadaiwa kuwa Mbowe alikuwa akiwasiliana
na wenzake kupitia mitandao ya Telegrama na kabla ya kukutekeleza
kitendo hicho washtakiwa walikamatwa.
Ameeleza kuwa mshtakiwa
Adam Kusekwa Mohamed Lingwenywa walikamatwa eneo la Rau wakiwa katika
harakati za kumsababishia Sabaya majeraha na mshita pili alipopekuliwa
alikutwa na siraha aina ya Pisto yenye Pastola tatu ambazo zilikuwa na
nia ya kutumika katika vitendo hivyo.
Washitakiwa hao
walisafirishwa hadi Dar es Salaam na walipohojiwa walikiri kujihusisha
na vikao mbalimbali vya kigaidi na walimtaja mshtakiwa Khalfan Bwire na
Mbowe kuwa sehemu ya wahalifu.
Agosti,9 mwaka 2020 mshitakiwa
Hassan Bwile , alikamatwa eneo la Changa'ombe na walipohojiwa katika
kituo cha polisi Chang'ombe alikiri kuhusika katika kikao cha kutekeleza
vitendo vya kigaidi.
Wakili amedai mshitakiwa Bwile
alipopekuliwa katika makazi yake eneo la Yombo alikutwa na mali za
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
pamoja na kidaftari kidogo na baada ya upekuzi fomu ya upekuzi ilidaiwa
na kushikwa mshitakiwa
Amedai kuwa kidaftari hicho
kilipopelekwa katika maabara ya maandishi ilibainika kuwa mwandiko
ulikuwa katika daftari hilo ni sawa na mwandiko wa mshitakiwa huyo.
Pia
Agosti 11 mwaka 2020 Luteni Urio aliwasilisha simu yake aina ya Tecno
katika maabara ya makosa ya mtandao kwa ajili ya uchunguzi na kuaminika
kwamba meseji za mawasiliano zilizokuja katika mtandao wa Telegram
kati Mbowe na Urio zilipatikana katika simu hiyo.
Amedai Jeshi
la Polisi liliendelea na uchunguzi na Julai 20 mwaka huu Mbowe
alikamatwa Mtaa wa Ghana ,Mwanza na kuunganishwa na washitakiwa wenzake
ambao ni Bwire Kasekwa na Lingwenya
Baada ya kusomewa maelezo
hayo, washitaliwa hao kupitia wakili wao Kibatala, mshtakiwa wa kwanza,
wapili na watatu walikubali majina yao na anwani zao.
Pia
washtakiwa hao wamekubali walikuwa watumishi wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania kama Makomandona na Ajira zao zilisitishwa kwa sababu ya
vitendo vya utovu wa nidhamu.
Washitakiwa hao wamekiri kufanya kazi pamoja katika kikosi cha Jeshi Ngerengere mkoa wa Morogoro na kwamba wanafahamiana.
Kwa
upande wa mshtakiwa Freeman Mbowe), amekubaliana na majina na anwani
yake ya makazi na kwamba ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema.Mbowe
amekiri kukamatwa Mtaa wa Ghana ,Iremela Mkoani Mwanza.
Awali
Wakili wa Utetezi Peter Kibatala alitaja kwa majina mashahidi saba pekee
huku wengine wanne akiomba mahakama kutoa kibali kwani baadhi yao ni
maafisa wa polisi na hivyo wanaweza kufikiwa kabla ya kutoa ushahidi
wao mahakamani hapo ombi ambalo limepingwa na upande wa Jamhuri.
Hata
hivyo, Jaji Siyani amesema, amesikiliza hoja za pande zote mbili
amekubaliana na ombi la kibatala licha ya kuwa sheria hairuhusu ila
inatoa mamlaka kwa mahakama kutoa uamuzi endapo kunakuwa na mazingira
yanayolazimisha mashahidi kufichwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Spetembe15 kwa ajili ya Kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa Jamuhuri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...