KATIBU
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) Taifa Itikadi na Uenezi
Shaka Hamdu Shaka amewaeleza viongozi na watendaji wote ndani ya Chama
na Serikali kushughulika na changamoto za wananchi badala ya kukaa
ofisini.
Shaka ameyasema hayo akiwa ziarani wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Pamoja
na mambo mengine ziara hiyo imelenga kuhamasisha na kuimarisha uhai wa
chama kuanzia ngazi ya shina, kuhimiza mahusiano ndani ya chama pamoja
na serikali.
Shaka ameendelea kuwahakikishia wananchi kuwa CCM na
serikali vipo salama na imara katika mikono ya Mwenyekiti na Rais
mahiri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan.
"Hii ni kwa sababu katika muda mfupi serikali
anayoiongoza imetoa mwelekeo wenye matumaini makubwa ya kuimarisha
ustawi wa wananchi, uchumi wa nchi yetu, kuvutia uwekezaji zaidi,
kuzalisha ajira kwa vijana na kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya
Nchi yetu na raia wote,"amesema Shaka
Shaka amewataka viongozi na
watendaji wote ndani ya serikali kuchapakazi kwani Chama, Rais Samia na
wananchi wanataka matokeo yanayoonekana na yanayopimika kutoka kwenye
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Wakati huo
huo Shaka ameilekeza Wizara ya Nishati kuhakikisha wanamaliza tatizo la
kukatikakati kwa umeme linaloendelea maeneo mbalimbali nchini ikiwemo
Wilaya ya Nachingwea.
Shaka pia amewataka wananchi kujitokeza
kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi
itakayofanyika mwaka 2022. Alihimiza serikali inatumia gharama kubwa
kukamilisha zoezi hilo kwani taarifa zake zina umuhimu mkubwa katika
kusukuma maendeleo ya nchi mbele zaidi hivyo ni muhimu kila mmoja
kulishiriki.
Shaka yupo kwenye ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa
iliyopo kwenye ziara mkoani Lindi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM
Daniel Chongolo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...