Na Cde. Msuya
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Dkt. Philisi M. Nyimbi (MNEC), akiwa katika Ziara ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM katika Mkoa wa Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe, amepokea Kilio cha wananchi wa Mchinga kupitia Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Salma R. Kikwete cha kuomba wapatiwe Halmashauri, afikishe ombi lao kwa Viongozi wa Juu wa CCM wenye Serikali iliyoko madarakani.
Akitoa Hotuba yake baada ya kumaliza ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa Maabara na Choo katika Shule ya Mvuleni - Mchinga, Dkt. Nyimbi aliwaeleza dhamira ya Ziara kuwa ni Kuwapongeza kwa wanachama na wananchi kwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na kupelekea CCM kuibuka na Ushindi kwa nafasi ya Rais wa JMT, Mbunge na Madiwani wa Jimbo la Mchinga.
“ Hongereni sana hasa kwa kutuletea Mbunge Mwanamke, hapa mmeongeza usawa wa kijinsia na Mhe. Salma Kikwete ni mchapa kazi” aliongea Dkt. Nyimbi.
Dkt. Nyimbi aliwasisitiza watendaji kusimamia uhai wa Chama hasa kukaa vikao vya kikatiba, ushirikiano, ulipaji wa ada, kuingiza wanachama wapya ambapo katika ziara yake hiyo alimpokea Kada Mkubwa mwanachama wa ACT Wazalendo aliyeamua kujiunga na CCM, Ndg. Abraham Chuma.
“Nimefurahi Serikali ya CCM inavyotekeleza Ilani yake hasa katia mikakati ya barabara nami sina sababu ya kubaki upinzani, nimeamua kujiunga na CCM” alieleza Ndg. Chuma.
Dkt. Nyimbi alieleza umuhimu wa zoezi la SENSA itakayo fanyika mwakani 2022, kuwa ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kifungu cha 206. Sensa inalenga kupata Takwimu ambazo Serikali ya CCM itazitumia katika kugawa Rasilimali za Taifa katika maeneo kulingana na mahitaji ya eneo husika katika mahitaji ya huduma za Afya, Elimu, Barabara, Ajira, Maji, Masoko.
“ Niwaombe mkawe mabalozi wazuri juu ya zoezi la Sensa, mkahamasishe watu washiriki kuhesabiwa ili serikali iwe na Takwimu sahihi zitakazo saidia katika kupanga maendeleo” Alisisitiza Ndg. Nyimbi.
Katika Swala la Vikao vya Mashina Ndg. Nyimbi alieleza kuwa kwa Mujibu wa Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 toleo la 2020, inatambua kuwa kikao cha kwanza cha CCM kitakuwa ni Shina.
“Ndugu Katibu wa Shina na Mweneyekiti hakikisheni vikao vinafanyika na mnaboresha rejesta ya wajumbe wenu ili kujua wajumbe hai” Alisisitiza Dkt Nyimbi.
Kuhusu Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Mchinga, Dkt. Nyimbi alimuomba Mbunge wa Jimbo Kuelezea Mafanikio na Cha
ngamoto, ambapo Mhe. Salma Kikwete alieleza jinsi Serikali ya CCM ilivyotekeleza Ilani kwa kuleta Jumla ya Fedha Milioni 349 za barabara ya Mchinga - Kijiweni, Bilioni 4 za ujenzi wa Shule ya Mchinga, Milioni 250 kwa ajili ya Afya pamoja na zaidi ya Milioni 30 katika shule ya Sekondari Mvuleni.
Mhe. Salma Kikwete akaelezea pia changamoto kubwa ni hitaji la Halmashauri ya Mchinga na Uharibifu wa Mazao kutoka kwa wanayamapori hasa Tembo na Nyani.“ Ndugu Katibu Mkuu tunaomba utufikiahie kilio hichi kwa Viongozi wakuu wa CCM cha uhitaji wa Halmashauri ya Mchinga ili kuweza kutatua Changamoto nyingi” Alisisitiza Mhe. Salma Kikwete.
Dkt. Nyimbi alipokea kilio hicho cha wakazi wa Jimbo ka Mchinga na Kuahidi kufikisha kwa viongozi wakuu wa CCM, kwani pia jambo hilo lilielezwa na Wazee wa Jimbo hilo ikiwa ni pamoja na Changamoto kadhaa katika utolewaji wa huduma za Afya na upatikanaji wa maji Mchinga.
Akihitimisha hotuba yake Dkt. Nyimbi aliwashukuru sana viongozi hao na kuwasisitiza waendelee kuchapa kazi, kumuunga mkono Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa. Pia kuendelea kuchukua Tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko hasa UVIKO-19.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...