Na Khadija Seif, Michuzi Tv

SHINDANO la kumtafuta mlibwende ukanda wa Pwani (Miss Easter zone)  linatarajia kufanyika Septemba 24 mwaka huu katika ukumbi wa Daynastic beach Ununio, Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi  wa Habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa shindano hilo, Nancy Matta amesema mshindi wa kwanza wa Kinyang'anyiro hicho atajinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu, huku mshindi wa pili akipatiwa shilingi milioni mbili na  nusu na kwa  Mshindi wa tatu Shilingi milioni moja.

Nancy ameeleza kuwa shindano hilo limeweza kupata washiriki kupitia Mikoa ya Pwani ipatayo minne.

 Aidha amesema kuwa, kutokana na nafasi yake na uzoefu wake katika mashindano hayo anaamini kuwa shindano hilo litakua ni sehemu ya washiriki kupata tiketi ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.

"Shindano  limeshirikisha Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani ambapo washindi watapata nafasi ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania na kuwakilisha taifa katika shindano la dunia." amesema.

Mratibu huyo ameongezea Kuwa Septemba 22 mwaka huu kutafanyika shindano la kumtafuta warembo wenye vipaji’ Miss Talent’.

"Shindano hili litafanyika mkoani Morogoro, nawaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia vipaji lukuki kwa warembo hawa." amesema.

Kwa upande wake Afisa Habari wa bodi ya Utalii, Maria Mafie amesema shindano hilo litasaidia kukuza na kuendeleza utalii wa ndani.

Maria amefafanua kuwa ugonjwa wa corona umesababisha kupungua kwa watalii nchini, hivyo shindano hilo litasaidia kuhamasisha watanzania kujitokeza katika vivutio.

Mratibu wa Shindano la Miss Easterzone Nancy Matta akionyesha crown ya atakaibuka Mshindi wa Shindano Hilo akiwa pamoja na wadhamini mbalimbali akiwemo mtengenezaji wa crown hiyo Amina Swedy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...