Raisa Said,Lushoto.


Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro amesema kumekuwa na wizi na udanganyifu kwenye mageti ya kukusanyia ushuru jambo ambalo linakwamisha halmashauri kukusanya mapato ya ndani  ipasavyo kutokana na hali hiyo iliyopo wilayani humo

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika ukumbi wa halmashauri,alisema tayari suala hilo la wizi  ameshalikabidhi kwa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Rushwa Takukuru kwaajili ya uchunguzi zaidi.

"Nilifanya ziara ya kushtukiza majira ya saa 2 usiku na kujione Udanganyifu unaofanywa na Vibarua na Supervisor katika geti la kukusanyia ushuru lililopo Nyasa" Alisema Mkuu wa Wilaya huyo.

 Alisema katika Geti  hilo la Nyasa alikuta kuna Mashine Nne (4) za POS na moja tuu ndiyo ilikuwa inatumika huku Vibarua aliowakuta wakitumia Daftari kuwekea rekodi za Ushuru na kutumia Namba ya Tigo ya Mtu binafsi/mmoja wa Vibarua aliowakuta kufanyia malipo ya Ushuru wa Halmashauri .

Wakati huo huo Mkuu  wa Wilaya huyo alitumia fursa hiyo  kunyooshea Kidole Kitengo cha Manunuzi kwa kushindwa kutimiza Majukumu na Wajibu wake ipasavyo  huku akianisha Ubadhilifu wa Fedha za Umma unaofanyika kwenye Ununuzi wa Vipuli vya Magari na Matengenezo ya Magari.

"Mfano gari la Halmashauri aina ya Isuzu FSR lilikuwa na tatizo la Difu alafu likashushwa Injini ili kuongeza gharama za matengenezo na gari la Kubebea Wagonjwa la Kituo cha Afya Kangagai ilipelekwa kwenye Matengenezo Tanga lakini likarudi likiwa bado ni Bovu" Alieleza Mkuu huyo wa wilaya huku akiongeza kuwa hata Ujenzi wa Kituo cha Mama na Mtoto ambao umeshatumia zaidi ya Milioni 400/= lakini  nbado Ujenzi haujakamilika na umesimama huku Mchakato wake wa Manunuzi ukigubikwa na Tuhuma za Rushwa.

Kalisti alisema Utekelezaji wa Miradi ya Serikali kupitia mfumo wa "Force Account" usiwe Kigezo cha Kufuja Fedha za Serikali zinazotumika kwenye Miradi hiyo kwa Kigezo cha "Kutokuingiliwa

Pia Mkuu  huyo wa Wilaya alisisitiza Miradi yote ya Maendeleo inayofanyika kwenye Kata, Vijiji Taarifa kamili za Utekelezaji wa Mradi husika lazima zifike kwenye Ofisi ya Diwani na Afisa Mtendaji Kata kwa kuwa itaondoa Malalamiko ya kwamba kuna Miradi ya Serikali inafanyika kwenye Kata bila wahusika.

Kalisti alisisitiza kuhusu swala la Mahusiano katika Utendaji Kazi na kuwasihi Madiwani na Watumishi kuwa na Mahusiano mazuri na hii itachangia kupunguza Migogoro kazini na kuongeza Ufanisi katika kuwatumikia Wananchi. 

Hata hivyo kwakuwa ndio mara yake ya Kwanza kushiriki kikao hicho tangu kuteuliwa kwake ,alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo ameahidi kufanya kazi kwa Uaminifu na Bidii kwa Kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge, Madiwani na Watumishi wengine wa Serikali kuwaletea Wananchi  Maendeleo ..."

Pia alimpongeza January Makamba (MB) wa Jimbo la Bumbuli kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati pamoja  na kuwapongeza Wabunge Shaban Shekilindi (MB) Jimbo la Lushoto na Husna Sekiboko (MB) Viti Maalum Mkoa wa Tanga kwa Kuhudhuria Vikao vya Baraza la Madiwani kama Wajumbe.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...