Na John Walter-Hanang
Mkuu
wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja amewaomba viongozi wa
dini wilayani hapo kuendelea kusimamia malezi na makuzi ya Vijana ili
kuwa na Taifa lenye hofu ya Mungu, Uadilifu na Uzalendo.Ametoa
ombi hilo katika mkutano wa 45 wa Mwaka wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Mbulu uliofanyika Wilayani hapo
ambapo amewashukuru na kulipongeza kanisa hilo kwa huduma nzuri
wanazotoa katika hasa katika huduma za Afya na Elimu kwani wanaunga
jitihada za Selikali kwa vitendo.
Aidha amewahakikishia Serikali ya Wilaya itaendelea kutoa ushirikiano kwao ili kufikia malengo ya kanisa.
Mkutano
huo uliongozwa na Baba Nicolaus Nzangazelu wa Dayosisi ya Mbulu
Nicolaus na kusimamiwa na Baba Askofu Michael Adam wa Dayosisi ya
Mara na Watumishi wa Mungu zaidi ya 300 kutoka Wilaya za Mbulu,
Hanang,Babati na Wilaya za jirani.
Baba
Askofu Nicolaus Nzangazelu amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kushiriki
katika Mkutano huo na ameahidi kushirikiana na Serikali ya Wilaya katika
kuimairisha huduma za jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...