MAHAKAMA Kuu kitengo cha uhujumu uchumi imeahirisha kuendelea kusikiliza ushahidi wa Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake kwa ajili ya Kusikiliza mapingamizi mawili yaliyowasilishwa na Upande wa Utetezi unaongozwa Wakili Peter Kibatala ukipinga maelezo ya Onyo kwa mshatakiwa wa wa Pili Adam Kusekwa Kuwasilishwa Mahakamani kama Ushahidi.

Hatua hiyo inakuja baada ya upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wao Peter Kibataka kupinga mahakama isipokee maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili ambayo yalipaswa kutolewa mahakamani hapo kama kielelezo na shahidi wa kwanza wa upande wa Mashtaka ambaye ni Kamanda ya Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, RPC Ramadhani Kingai.

Wakili Kibatala amedai Kuwa maelezo Hayo hayakidhi vigezo vya Kutumika Mahakamani Kama Ushahidi Kwa kuwa wakati Mshatakiwa anachukuliwa maelezo yake aliteswa zoezi na kuteswa kwake Liliongozwa na ACP Ramadhani Kingai na Maafisa Wengine wa Polisi

Akipinga kupokelewa kwa maelezo hayo, Kibatala amesema, mshtakiwa alichukuliwa maelezo nje ya muda wa kisheria ilivyoelekezwa kwamba maelezo yamechukuliwa zaidi ya masaa manne tangia akamatwe, maelezo yamechukuliwa nje ya muda hivyo hayawezi kupokelewa mahakamani hapo.

Pia amesema mshtakiwa kabla ama wakati akichukuliwa maelezo aliteswa zoezi ambalo lilisimamiwa na Shahidi Kingai pamoja na maafisa wengine wa upande wa mashtaka.
Kesi hiyo inaendelea saa nane mchana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...