Charles James, Michuzi TV
NASIMAMA na Samia! Hii ni kauli ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ambaye ameitoa leo kufuatia kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kuwa atagombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao 2025.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokua akizungumza na Wanawake katika Siku ya Demokrasia duniani ambayo maadhimisho yake hufanyika kila mwaka ifikapo Septemba 15,2021 hapa nchini maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Rais Samia amesema, "Wanawake wa watanzania hawajamueka Rais wa Kike Tanzania Ila ni kudra za Mwenyezi Mungu na Katiba tu, Lakini watanzania watamueka Rais mwanamke 2025 kwani atachukua fomu ya Urais, wameanza kutuchokoza eti Samia hatochukua fomu nani kasema?.
Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri tukishikamana, tukimuweka Rais wetu tutakutana hapa Kwa furaha kubwa sana, kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama, nani kawaambia?" Amesema Rais Samia.
Kufuatia kauli hiyo Mbunge Ditopile ametoa maoni yake akisema yeye kama Mbunge mwanamke na mtanzania anamuunga mkono Rais Samia kugombea Urais 2025 kwani ni nafasi ambayo imejitokeza kutokana na kudra za Mwenyezi Mungu.
"Rais Samia amekua muwazi kuwa nafasi aliyopata imetokana na kudra za Mwenyezi Mungu na Katiba, hadi sasa ameonesha mwanga na utendaji wa hali ya juu katika kuwatumikia watanzania, nipo nyuma yake mwaka 2025 atakagombea Urais.
Sisi kama Wanawake wa Tanzania hatuna budi kumuunga mkono Rais wetu, hii ni nafasi yetu tumeona namna anavyowapa nafasi nyeti Wanawake katika kuonesha uwezo wao, mimi Ditopile nasimama na Samia 2025." Amesema Ditopile.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...