Mkuu wa Wilaya ya Hanang  Janeth Mayanja.akizungumza kwenye  mkutano wa 45 wa  Mwaka wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Dayosisi ya Mbulu uliofanyika wilayani hapo jana. Katikati (mwenye barakoa nyeusi) ni Baba Askofu  Michael Adam wa Dayosisi ya Mara.


   Baba Askofu  Nicolaus Nzangazelu wa  Kanisa hilo Dayosisi  ya Mbulu akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang  Janeth Mayanja.

Watumishi wa Mungu wa kanisa hilo wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano huo ukiendelea. 



Na Mwandishi Wetu, Hanang.

MKUU wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja amewaomba viongozi wa dini wilayani hapa  kuendelea kusimamia malezi na makuzi ya vijana ili kuwa na Taifa lenye hofu ya Mungu, uadilifu na uzalendo.

Mayanja Amametoa ombi hilo jana wakati akizungumza kwenye  mkutano wa 45 wa  Mwaka wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Dayosisi ya Mbulu uliofanyika wilayani hapo jana.

Mayanja alitumia nafasi hiyo kulishukuru kanisa hilo kwa kuunga jitihada za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kutoa huduma nzuri kwa jamii.

"Niwapongeze kwa shughuli mbalimbali mnazozitoa kwa wananchi hasa  katika sekta ya Afya na Elimu kwani mnaunga jitihada za  Selikali kwa vitendo". alisema Mayanja.

Aidha amelihakikishia  kanisa hilo kuwa Serikali  wilayani humo  itaendele kutoa ushirikiano kwa Dayosisi hiyo  ili kufikia malengo yao ya kukuza uchumi na utoaji wa huduma za kiroho.

Baba Askofu  Nicolaus Nzangazelu wa  Kanisa hilo Dayosisi  ya Mbulu  amemshukuru mkuu wa wilaya hiyo  kwa kushiriki katika mkutano huo na ameahidi kushirikiana na Selikali katika kuimairisha huduma za jamii.

Mkutano huo uliongozwa na Baba Askofu  Nzangazelu  na kusimamiwa na Baba Askofu  Michael Adam wa Dayosisi ya Mara na kuhudhuriwa na watumishi wa Mungu zaidi ya 300 kutoka Wilaya za Mbulu, Hanang, Babati Vijijjni na wilaya za jirani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...