Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 13 Septemba, 2021.


Na Avila Kakingo, Globu ya Jami
JAJI Mkuu wa Serikali, Profesa Ibrahim Juma amwagia sifa Mwanasheri Mkuu wa Serikali, Dkt. Elizer Mbuki Feleshi aliyechukua nafasi ya Profesa Adelardus Kilangi.

Akizungumza mara baada ya Kuapishwa kwa wabunge wateule na Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo Septemba 13,2021 ya Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa Dkt. Elizer Mbuki Feleshi ni mtiifu kwa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtiifu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada alaipopata wito wa kuhudhuria kikao cha leo.

“Dkt. Elizer Mbuki Fereshi ambaye nimefanya naye kazi tangu Juni 4, 2018 hadi leo alipopata kiapo chakuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mujibu wa Ibara 109 ibara ndogo ya 2 huyu alikuwa msaidizi maalumu katiba inatumia Luhga hiyo kuwa msaidizi maalumu wa jaji mkuu ambaye anasimamia uendeshaji wa mahakama kuu na mahakama ambazo zipo chini ya mahaka kuu ambazo zinabema asilimia 80 ya mashauri yote ambayo yanasikilizwa katika mahaka za Tanzania.” Amesema Prof Ibrahim

Prof. Ibrahim amesema kuwa Dkt. Feleshi ni mtu wa maboresho kwani anapenda Tehama na anaitumia kikamilifu katika kusimamia mahakama ambazo zimetapakaa nchini kote.

“Bila Tehama usimamizi wa Mahakama ungekuwa Mgumu san asana.” Amesema Prof. Ibrahim

Amesema kuwa Dkt. Elizer Mbuki Feleshi alikuwa anasimamia, kila siku chai yake ya asubuhi ni kuangalia mashauri mangapi yamesajiliwa, mashauri mangapi yametolewa hukumu, mlundikano wa mashauri upo katika hali gani, mahakama gani imebeba mzigo mkubwa zaidi.

“Ni mfatiliaji lakini ni Mfatiliaji kwa kutumia Teknolojia, vile vile yeye ametajwa katika kusaidia watumishi wa chini yake, anauwezo wa kutumgundua Talent, na kuzijenga na kuziendeleza, naamini atasaidia sana katika nafasi yake ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.” Amesema Prof. Ibrahim

Licha ya hayo Pro.Ibrahim amesema kuwa ni mwadilifu kwani alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili ya maafisa wa mahakama na ameifanya vizuri. Amesema kwenye suala la Uadilifu hana shaka naye.

Dkt. Elizer Mbuki Feleshi ni mtu anayependa maendeleo na huleta mrejesho, ni mtu ambaye ni mfuatiliaji sana.

Nawakabidhi muweze kumtumia ikifika wakati wa kumrudisha tupo teyari kumpokea.” Amesema Prof. Ibrahim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...