Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
Mashua
ijulikanayo kama ‘MV Adui Jamaa (Mbagara)’ imepata ajali na kuzama
katika eneo la Simani (Songosongo) huko Mafia juzi,na kusababisha vifo
vya watu watatu na wengine wawili bado hawajapatikana kuokolewa.
Mashua hiyo ilikuwa na mzigo wa mwani ikiusafirisha kutoka kisiwa cha Jibondo wilayani Mafia kuelekea Kilwa.
Jumla ya watu sita walikuwa katika mashua hiyo ambapo wanne kati yao walikuwa ni wafanyakazi na wawili ni abiria.
Mkuu
wa wilaya ya Mafia Eng. Martin Ntemo alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo ambapo mara baada ya kupokea taarifa hizo za kusikitisha aliviagiza
vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kwa kushirikiana na wadau
wengine, kwenda katika eneo ilipotokea ajali ili taratibu za uokoaji
zichukuliwe mara moja.
Aidha
abiria mmoja aliyetambulika kwa jina Saidi Twalibu aliokolewa akiwa
hai,ambapo Wataalam kutoka Hifadhi ya Bahari Mafia (HIBAMA) waliongoza
zoezi la uokoaji.
Msako huo umedumu kwa siku tatu mfululizo tangu ajali itokee hadi maiti tatu zilipopatikana maeneo ya Rufiji na Kilwa.
Miili
iliyopatikana imetambuliwa kuwa ni Amri saidi Amri (Ngenje) aliyekuwa
nahodha wa chombo kilichopata ajali na Sadiki Abdallah Apondo ambao wote
wamepatikana na kuzikwa katika kijiji cha Pombwe wilayani Rufiji.
Mwili mwingine ni wa Selemani Faki Hassani (Mnyaku) ambaye anazikwa katika kijiji cha Somanga wilayani Kilwa.
Jitihada
zinaendelea za kuwatafuta wahanga wengine wawili ambao ni Hamza Shahame
na Ahmadi Mwinyimanga, hatma yao bado haijajulikana.
Mkuu
wa Wilaya ya Mafia,Ntemo alielezea kusikitishwa kwake kwa kutokea ajali
hiyo na anaungana na ndugu na jamaa wote waliopoteza wapendwa wao.
Ntemo
amewasihi wamiliki na maendesha vyombo vya usafiri majini kuhakikisha
wanazingatia masuala ya usalama hasa kwa kutozidisha uzito, kukagua mara
kwa mara ubora wa vyombo vyao na kufuata miongozi mbali mbali
inayotolewa na wataalam ikiwa nipamoja na hali ya hewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...