JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wahalifu zaidi ya 152 kwa tuhuma za kujihusisha na makosa ya kijinai jijini Dar es Salaam.
Ikiwa Jeshi la polisi likiendelea na jitiada za kusimamia mifumo ya kuzuia na kupambana na vitendo vya kihalifu kwa kufanya operasheni maalum za kupambana na wahalifu zenye kulenga makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, madawa ya kulevya ya shambani na viwandani na wahalifu wengine wanaotenda vitendo ambavyo ni kero kwa wananchi.
Katika taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Muliro Mumanne Muliro imeeleza kuwa Wahalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha 17 walikamatwa na vielelezo ambazo ni pikipiki 03, wahalifu wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya ya shambani na viwandani walikamatwa watuhumiwa 39 na vielelezo kama ifuatavyo:-
Viroba vya bhangi 12 Kete za bhangi 1,005 Madawa yadhaniwayo ya kulevya aina heroini pakiti 05 Pia, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam liliwakamata wahalifu wengine 97 wanaotenda vitendo vya uvunjaji na ukwapuaji ambavyo ni kero kwa wananchi na walikamatwa na vielelezo mbalimbali.
Simu za mkononi 30 Komputa 01 Televisheni za aina mbalimbali 08 vitu vingine ni redio, spika, deki n.k
Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia mfumo wa ushirikishwaji wa jamii katika kutanzua uhalifu kikundi cha polisi jamii kilichopo buguruni madenge kilifanikiwa kukamata silaha moja bastola aina ya Browning ikiwa na risasi nne ndani ya magazine.
Kikundi hicho mnamo tarehe 05/09/2021 majira ya saa saba usiku kikiwa doria mtaa wa Buguruni Magengeni kiliwatilia mashaka watu watatu na kuanza kuwafuatilia ndipo watu hao walipokimbia na kutupa begi dogo la mgongoni na polisi jamii walipolipekuwa begi hilo walikuta vitu.
Hata hivyo wamekamata Silaha moja bastola aina ya browning Spana aina pipe ranger 1 Prize kwa ajili ya kukatia makufuli Uchunguzi wa Jeshi Polisi umebaini silaha hiyo iliibiwa tarehe 02/08/2021 majira ya usiku huko kawe kilongawima nyumbani kwa Max Kaniti Mlelwa,(48),Mfanyabiashara,ambaye ndiye mmiliki halali wa silaha hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...