KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Ramadhan Kingai amekana kumtesa mshitakiwa Adam Kusekwa kabla au baada wakati wa kuandika maelezo yake ya onyo kama upande wa utetezi unavyodai.

Kingai ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka katika kesi ndogo ndani ya kesi ya Msingi  ambaye pia ni shahidi wa kwanza katika kesi ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake .

Ameeleza hayo leo Septemba 15,2021 katika Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Mustafa Siyani, wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo ndogo kufuatia mapingamizi ya upande wa utetezi wakipinga kupokelewa kwa maelezo ya onyo ya mshitakiwa huyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wao Peter Kibatala kupinga Mahakama isipokee maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili Adam Kusekwa, yaiyopaswa kutolewa mahakamani hapo kama kielelezo na shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka ambaye ni Kamanda ya Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, RPC Ramadhani Kingai.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Robert Kidando Kingai amedai mshtakiwa Kusekwa  hakuteswa na wala hawakuwa na haja ya kufanya hivyo kwani hata wakati wa ukamatwaji Polisi hawakutumia nguvu.

Kamanda Kingai amedai hakukuwa na sababu ya kumtesa mshtakiwa kwani hata baada ya kuwakamata wao bado walikuwa na uhitaji wa kuwakamata watuhumiwa wengine na walikuwa wanahitaji  msaada  wao ili kuwapata washtakiwa wengine.

Amedai mazingira ya kumkamata yalikuwa ya kawaidia na hata wakati wa kusafiri kutoka Moshi kuja Dar es Salaam hakukuwa na shida yoyote  na alitoa maelezo akiwa huru.

Pia Kingai amedai wakati wa kuwakamata washtakiwa walidhani kungeweza kutokea mazingira magumu kwa kwa kuwa walikuwa ni askari lakini hali ilikuwa tofauti na hakukuwa na shida yoyote.

Akijibu maswali  ya Wakili wa utetezi Pater Kibatala kama kuna mahali popote ambapo alionesha washtakiwa katika kipindi chote walichokamatwa  hadi kuwahoji kama walipewa chakula jambo ambalo Kamanda Kingai amedai hakuna mahali aliposema washtakiwa walipewa chakula kwa kipindi chote hicho.

Pia Wakili  Kibatala alimuuza shahidi kama mshtakiwa Kusekwa  aliwahi kumweleza kama anamatatizo ya afya yanayoshabihiana na ugonjwa  wa akili (Stress) ,Kamanda Kingai amedai mshatakiwa aliwahi kumueleza ila hakufuatilia.

 Aidha, Kibatala amemuuliza Kingai kuwa ni kwa sababu gani   jalada la kesi dhidi ya washtakiwa lilifunguliwa Dar es Salaama  na maelezo ya  mashahidi wawili walioshuhudia upekuzi wa maungoni wakati wa kukamatwa kwa washtakiwa eneo la Rau Madukani  Moshi yalichukuliwa kituo cha polisi cha kati Moshi.

Shahidi amedai kuwa walifanya  hivyo kwa kuwa maelezo ya mashahidi yanaweza kuchukuliwa mahali popote na hata wangeweza kuandika palepale Rau madukani lakini hali ya pale ilikuwa hairuhusu.

Kufuatia hali hiyo shauri  limeahirishwa hadi  kesho ambapo itaendelea kwa upande wa Jamuhuri kumuhoji shahidi (Re examination)

Katika kesi hiyo ndogo ndani ya kesi ya msingi jumla ya mashaidi saba wanatarajiwa kutoa ushahidi kwa upande wa Jamuhuri.Mbali na Mshtakiwa Adam Kusewa, washtakiwa wengine ni Mohamed Lingwenywa, Hassan Bwire Hassan na Freeman Mbowe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...