Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia Bia yake ya Pilsner Lager, leo imewakabidhi washindi wawili wa kampeni ya ‘Kapu la Wana’ kutoka mikoa ya Morogoro na Njombe vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kila mmoja.
Kupitia kampeni ya ‘Kapu la Wana’, bia ya Pilsner imetenga kiasi cha shilingi milioni 50 ambazo zitatolewa kwa washindi watano ambapo kila mmoja atajishindia vifaa kwa ajili ya kukuza biashara yake vyenye thamani ya shilingi milioni 10.
Jackline Lola Minja (30) mkazi wa Morogoro mjini na amiliki studio ya picha pamoja na Rehema Lawrence Mbuya (29) mkazi wa Njombe na mmiliki wa duka kuuza pemejeo, wamekuwa ndiyo washindi wa pili na watatu wa kampeni ya ‘Kapu La Wana’ baada ya mshindi wa kwanza kutoka wilayani Muleba kupatikana na kukabidhiwa zawadi ya Power tiller mwisho mwa mwezi Agosti.
Jackline kutoka Morogoro amekabidhiwa vifaa vya studio ikiwamo kamera, kompyuta, printa na vinginevyo vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kupanua biashara yake wakati Rehema akikabidhiwa gari la kubeba mizigo aina ya Carry kwa ajili kumsaidia kupeleka mizigo ya wateja wake.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi hao, meneja chapa wa SBL Ester Raphael alisema zawadi zilizotolewa ni muendelezo wa kampeni hiyo inayolenga kuwawezesha vijana wajasiriamali wapambanaji kufikia malengo yao kupitia Bia ya Pilsner.
“Pilsner, bia ya wapambanaji, leo inawazawadia wapambanaji wawili vifaa kwa ajili ya kukuza biashara zao. Siku chache zilizopita, tulishuhudia mpambanaji mwingine Privatus Mujuni kutoka Muleba Mkoani kagera naye akiwezeshwa pia. Kampeni bado inaendelea na kila mpambanaji ana nafasi ya kushinda, tuendelee kushiriki,” alisema Ester
Mshindi kutoka Morogoro Jackline Minja alisema changamoto kubwa aliyokuwa akikabiliana nayo ni ukosefu wa vifaa ambapo alikuwa akilazimia kukodi kamera na vifaa vingine kwa gharama kubwa na hivyo kujikuta akishindwa kupiga hatua.
“Nimekuwa nikishindwa kupiga hatua kwa kuwa vifaa vingi ninavyotumia ni vya kukodi. Faida ninayopata ni ndogo sana kwa kuwa kiasi kikubwa kinakwenda kwenye kukodi vifaa. Bia ya Pilsner imefungua kurasa mpya katika maisha yangu maana sasa vifaa ninavyo na sasa ndoto yangu ya kusimama imara zaidi na kusonga mbele inakwenda kutumia. Naishukuru sana bia ya Pilsner,”alisema
Kwa upande wake Rehema kutoka Njombe alisema changamoto kubwa aliyokuwa anakabiliana nayo ni ukosefu wa usafiri wa kufikisha mizigo kwa wateja na kusema gari alilopewa litamsaidai kuimarisha biashara yake na kumfanya asonge mbele kwa haraka zaidi.
“Nina kila sababu ya kuishukuru bia ya Plisner kuputia kampeni ya ‘Kapu la Wana’ kwa uwezeshaji huu mkubwa kwangu. Gari hili litanifanya niweze kuwahudumia wateja wangu vizuri zaidi kwa kuwafikishia mizigo,” alisema
Kwa mujibu wa Ester, shindano hilo ni mahususi kwa ajili ya vijana wapambanaji wanaofanya shughuli mbalimbali kama ukulima, uvuvi, vinyozi n.k. ambao wanatamani kufikia malengo makubwa lakini wanapata changamoto katika upambanaji wao kutokana na kukosa uwezeshwaji hali inayowapungizia kasi ya kufikia malengo yao na mafanikio kwa wakati.
“Pilsner ni bia ya vijana wapambanaji, wasiokata tamaa na wenye kiu ya kufikia mafanikio makubwa.Tumeona ni vyema kuwawezesha wateja wetu wenye kiu ya mafanikio kwa kuwapa vitendea kazi ili wazidi kusonga mbele zaidi.”
Alifafanua kuwa moja ya vigezo vitakavyotumika kupata washindi ni pamoja na umri usiozidi miaka 35 mshiriki atahitajika kuwa na biashara isiyozidi miaka miwili pamoja na kuwa na stori ya kuvutia juu ya namna alivyoanza na wapi anataka kuipeleka biashara hiyo.
“Tunatambua kwamba ujasiriamali na biashara si kitu rahisi. Unahitaji maono, uwekezaji na uvumilivu ili kupiga hatua. Kila mmoja ana namna yake ambayo ameweza kuanzisha biashara au kazi anayofanya sasa hivi, kwahiyo tunachokifanya ni kuchukua mawazo na stori bora zaidi ambazo zitaweza kuamsha ndoto za vijana wengine,” alisema Ester
“Unachotakiwa kufanya ni kufuatilia matangazo yetu katika vipindi mbalimbali vya redio na utashiriki kwa kupiga namba 0800750203 Bure Kabisa kisha kufuata maelekezo kutoka timu yetu maalumu ya wataalamu wabobezi, na baadaye utaweza kueleza biashara yako na namna ambavyo ungetamani bia yetu ya Pilsner ishiriki katika kukuza biashara yako,” alifafanua
Aliongeza “Kushiriki kwa njia ya baa, nunua bia yako ya Pilsner upate namba ya ushiriki. Mawazo bora 5, yataweza kupitishwa baada ya timu kujiridhisha na uhalisia wa shughuli ikiwamo kuwatembelea wapambanaji hao katika maeneo yao ya kazi,” alisema
Ester alitoa wito kwa Vijana wote wapambanaji wajitokeze kuchangamkia fursa hiyo itakayoweza kuwainua na kuwatoa hapo walipo kama alivyozawadiwa Jackline na Rehema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...