Na Anthony Ishengoma Ishengoma-Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amesema kuzimika kwa taa za Barabarani katika Manispaa ya Shinyanga kulileta sintofahamu kwa wananchi wa Shinyanga kutokana na athari za usalama wa biashara zao ulichangiwa na uwepo wa wahalifu waliotumia fursa ya kuzimika kwa taa hizo kufanya uhalifu.

Taa hizo za barabarani zilizimika kutoka na mkandarasi hapo awali kufunga taa za kutumia nguvu ya jua ambazo zilikuwa hazina ubora na kuzimika kwa kipindi kifupi baada ya kuwa zimefungwa na kuleta usumbufu kwa katika mitaa kwani biashara zilikuwa zinafungwa mapema saa kumi na mbili.

Akiongea na vyombo vya habari wakati wa zoezi la kufunga upya taa hizo Dkt. Philemon Sengati alisema uongozi katika Mkoa wa Shinyanga ulimtaka mkandarasi huyo kufanya marekebisho katika taa hizo na alikubali sharti hiyo na kwa kipindi kifupi sasa tayari taa zimeanza kufungwa.

‘’Wafanyabiashra katika eneo hili walilazimika kukodi taa kwa takribani elfu 15 kwa mwezi zile zenye mwanga mkubwa kutoka kwa wafanyabiashara baada ya taa za wali kuzima na palikuwa na sintofahamu’’. Aliongeza Dkt. Philemon Sengati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Dkt. Sengati aliongeza kuwa taa zilizokuwa hazifanyi kazi ni taa 428 ambazo mkandarasi amezifanyia marekebisho na amefanya hivyo kwani bado alikuwa anadai kiasi cha Tsh. Mil.200 ambazo aliambiwa kama atashindwa kusimamia zoezi hilo basi Mkoa usingetoa kiasi hicho cha fedha kama sehemu ya deni kwa mkandarasi huyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko alilitaja zoezi hilo kuwa sehemi muhimu la kiusalama kwani baadhi ya vibaka walikuwa wanatumia fursa ya giza kuleta usumbufu kwa wananchi ikiwemo wafanyabiashara wa mtaa wa sukari ambao walikuwa wanalazimika kufunga biashara mapema kuepuka usumbufu huo.

‘’Kikubwa walitakiwa kurudia taa zote 428 na mpaka sasa washabadilisha taa 400 na tunategemea leo watamaliza taa zilizobaki na wamekuwa wakibadilisha taa 60 kwa siku kwahiyo niseme wananchi wanaweza kufanya biashara zao usiku kucha kama wanaweza na wale wengine ambao walikuwa wanapata usumbufu mkubwa kutokana na taa kuzimika na wao wanaweza kuendelea na biashara zao’’. Aliongeza Bi. Jasinta Mboneko.

Baadhi ya Wananchi walipongeza hatua ya kurejesha tena taa hizo akiwemo Bi. Irene Mathias ambaye alisema kuwa kitendo cha taa hizo kuwaka sasa ataendesha biashara yake mpaka usiku lakini pia wasiwasi wake aliokuwa nao kuhusu kukabwa na vibaka haupo tena.

Wakati huohuo Msimamizi wa Tarura Mkoa wa Shinyanga Muhandisi Osward Girbert alikiri kuzimika kwa taa hizo na changamoto za kimkataba lakini sasa taa izo zimewaka na mkandarasi alilazimika kufanya marekebisho kwa kuagiza betri mpya na hivyo kurejesha huduma hiyo na hivyo anashukru kurejea kwa huduma hiyo.

Mfanyabiashara ndogo aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Cyprian alisema kabla ya marekebisho ya Taa alikuwa hawezi kufanya biashara yake kwa kipindi kirefu kwani alikuwa anatumia taa za kuchaji lakini sasa kutokana na kuwepo kwa mwanga wa kutosha ataweza kufanya biashara kutegemea mwanga wa Taa hizo na hivyo kufanya biashara yake vizuri.

Benki ya Dunia ilitoa msaada wa kujenga mtandao wa Barabara za lami Manispaa ya Shinyanga takribani kilomita 13 na serikali kupitia Tarura iliweka mkandarasi kufunga taa ambazo awali zilizimika kutokana na betri kutokuwa na ubora lakini zoezi linarudiwa ili kuleta ufanisi kati suala zima la kuhakikisha taa za barabarani zinarejea katika hali yake. 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akifuatilia kwa makini kujionea namna ambavyo mafundi wa kutenegeneza taa za barabarani za  umeme jua namna zunavyofanyakazi kutoka kwa moja ya mafundi wa kazi hizo jana katika mitaa ya Manispaa ya Shinyanga.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akifuatilia kwa makini akipata ushauri kutoka kwa Meneja wa Tarura Shinyanga Muhandisi Salvatory Amri wakati zoezi la kubadilisha taa za barabarani jana katika mitaa ya Manispaa ya Shinyanga pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akifuatilia kwa makini akipata ushauri kutoka kwa Meneja wa Tarura Shinyanga Muhandisi Salvatory Amri wakati zoezi la kubadilisha taa za barabarani jana katika mitaa ya Manispaa ya Shinyanga pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...