Na Humphrey Shao, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameagiza wafanyabiashara ndogondogo maarufu Machinga waliopo kandokando mwa barabara ya Kilwa eneo la Mbagala rangi tatu kuondoka mara moja kumpisha mwekezaji.
Makalla ametoa maagizo hayo leo alipokuwa akijibu kero za wananchi wa Jimbo la Mbagala ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Mkoa mzima wa Dar es Salaam kwa kutembelea jimbo kwa jimbo, ambapo akiwa eneo hilo amewaagiza Machinga hao kuondoka maeneo hayo.
"Sh.bilioni 217 zimetolewa kwenye miradi awamu ya tano kwa ajili ya mradi wa mwendokasi mbagala kwa urefu wa kilomita 12.3 ambayo utaleta afueni wa usafiri, hivyo siwezi kukubali mradi ukachelewesha kwa maslahi ya watu wachache ambao wanabiashara zao,"amesema Makalla.
Amewataka wafanyabiashara hao watoke wenyewe kwani watakaokadi wataondolewa kwa nguvu na kwamba mradi huo unachangamoto kubwa kwasababu ya wafanyabiashara wengi kila wanapotolewa wanarudi tena.
'Wakandarasi wanalalamika wananchi kufanya biashara maeneo ya miradi huo, kwanza ni hatari kwa sababu inaweza kusabisha majeraha na vifo endapo tatizo lolote litakalo jitokeza,"amesema.
Amesisitiza wananchi waruhusu wakandarasi wafanyakazi sehemu ya miradi hiyo wafanye vizuri waikamilishe “uhuru bila mipaka ni fujo”.
Aidha Makalla amewaomba pia wakandarasi wafanye kazi na kukamilisha kwa muda walioahidi kumaliza kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...