MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, ametoa wito kwa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar, kuhamasisha na kuelemisha wananchi kuendeleza maridhiano ya Serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo ni muhimu katika kusaidia kujenga amani ya nchi.
Mhe. Othman ameyasema hayo leo ofisini kwake Migombani alipozungumza na Uongozi wa Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA).
Amefahamisha kwamba hatua hiyo ni muhimu kwa kutasaidia katika kujenga amani ya kweli kwani bila ya kuwepo kunaweza kuchangia kuongezeka idadi ya watu wenye Walemavu .
Amesema ni muhimu ajenda ya kuhubiri suala hilo ikabebwa na kila mmoja ama taasisi miongoni mwa wanajamii na kila mmoja kujiona na muhusika wa kuhubiri serikali ya umoja wa kitaifa.
Aidha Mhe. Othman ametaka jamii kuachana na utamaduni wa kufanya mambo na matendo yanayoweza kusababisha ajali na kuongeza idadi ya walemavu.
“ Utakuta mtu anaendesha gari, ama baiskeli huku ana anasikiliza simu kwa kuwa anataka kumridhisha mtu mwengine na kusahau kwamba jambo hilo ni hatari na linaweza kusababisha ulemavu na kuongeza idadi ya watu wenye ulemavu” , alitanabahisha Mhe. Makamu wa Rais.
Aidha Mhe. Othman amewaeleza wanajumuiya hiyo kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na watu wenye ulemavu katika kusaidia kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Zanzibar Nd. Ali Omar Makame ame seshauri serikali kufanya utafiti makhususi ili kuibua na kufahamu sababu za kuongezeka tatizo la ulemavu Zanzibar.
Alisema kwamba kwamba pia kunahaja ya kuwepo jimbo la watu wenye ulemavu ili kupata uwakilishi sahihi zaidi wa watu wenye ulemavu katika vyombo vya kutunga sheria badala ya utaratiubu wa sasa kupitia kwenye vyama vya siasa.
Wakati huo huo , Mhe. Makamu wa Rais amekutana na kuzungumza na ujumbe wa Taasisi inayosaidia vijana kupata fursa za masomo nje ya nchi ya CARI VISION na kueleza kwamba vijana hao wanafanya jambo jema, lakini pia ni muhimu kuangalia mazingira ya vijana katika vyuo na taasisi wanazokwenda kusoma nje ya nchi.
Mhe. Makamu aliwataka Taasisi hiyo kuandaa mfumo bora zaidi utakaowezesha kuwasaidia vijana kupata elimu bora inayolingana na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
“ wakati mwengine mazazi anataka kujiridhisha kujua namna na hali ya elimu inayotolewa , mazingira ya kijana anavyoishi na mambo mengine ni vyema pia na hili likawa miongoni mwa mambo manayoyafanyia kazi” alitanabahisha Mhe. Makamu.
Naye Meneja wa Taasisi hiyo ya CARI
VISION yenye makao yake Makuu Mjini Dar es Salaam Yusuph Mohammed ameomba Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuwapa ushirikiano zaidi ili kuwasaidia vijana kupata
elimu nje ya nchi kwa ngazi na kada mbali mbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...