Na Linda Shebby
KAMISHNA Msaidizi Muandamizi  Mtaafu wa Jeshi la Polisi nchini SACP Jamal Rwambow leo amezindua kitabu chake  Kinachokwenda kwa jina Jamal Rwambow kinachozungumzia  maisha  ya Kachero wa Polisi.

Akizungumza leo katika uzinduzi huo  ulio fanyika kwenye ukumbi wa mikutani uliopo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam alisema kuwa kitabu hicho kitakua kikiuzwa kwa shilingi 25,000.
Aidha maudhui yaliyomo ndani ya kitabu  hicho ni pamoja na historia iliyojaa mafunzo visa na mikasa  ya ukachero.
"Katika kitabu hiki Kuna mambo mengi  ya kujifunza vijana pamoja na makachero kwa ujumla" alisema SACP Rwambow.

Alisema kuwa akipata msukumo wa kuandika kitabu hicho baada ya kung"amua kuwa  wapo watumishi wengi  wakiwamo makamanda ambao  wao wamefanya mambo mengi makubwa na kuitumikia nchi  lakini wamestaafu bila kufahamika hivyo nimeandika kitabu hiki huku lengo kubwa likiwa ni kutunza kumbukumbu,alisema Rwambow.
"Mimi ndiye niliweza kufanikiwa kukomesha mauaji y watu wenye Ualbino wakati nilipokuwa Kamanda wa Mkoa wa Mwanza (RPC), na nilifanikiwa baada ya kuweza kutumia mbinu zangu za kikachero kwa kuwatumia wanajamii kupata taarifa mbalimbali ambapo niliokuwa nikiwalipa kiasi Cha Mil1 huku aliyekuwa Mkuu wa Mkoa kwa kipindi kile Hayati Abbas Kandoro aliongeza kiasi cha pesaSh. Mil.1 hivyo msamaria mwema aliyeleta taarifa sahihi na Jeshi lilajiridhisha alikua akilipwa kiasi cha Sh. mil 2.
Naye Mhandisi Filbert Rweyemamu ambaye ndiye aliyeandika Dibaji ya kitabu hicho ametoa wito kwa  maofisa na maaskari ikiwemo raia kukinunua kitabu hicho kwa sababu Kuna mambo muhimu wataweza kujifunza.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...