Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Septamba 28, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  Dkt Hafez Ghanem Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amemuhakikishia Dkt. Ghanem kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika masuala mbalimbali ya kuinua uchumi hapa mnchini.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema kwamba serikali ya awamu ya sita imeweka kipaumbele katika kuinua sekta binafsi pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji hapa nchini. Amesema mpango wa maendeleo wa miaka mitano umelenga kuinua sekta ya viwanda hapa nchini hivyo serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kufanikisha hilo.

Aidha Makamu wa Rais Dkt. Mpango amesema ili kukidhi mahitaji ya sekta binafsi hapa nchini serikali imeweka mkazo katika sekta ya elimu hasa elimu ya ufundi ili kupata wahitimu wenye ujuzi watakaoweza kusaidia kuinua sekta hiyo.

Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kuimarisha utawala bora pamoja na kudhibiti rushwa hapa nchini hivyo kuweka mazingira rafiki ya kutekeleza miradi mbalimbali.

Kwa upande wake makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem ametaja maeneo ambayo benki hiyo itashirikiana na Tanzania ambayo ni pamoja na uboreshaji miundombinu, , mapambano dhidi ya uviko19 pamoja na kuinua uchumi baada ya janga la Uviko 19.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Septemba 28 , 2021.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor akiwa katika picha ya pamoja  na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao  Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Septemba 28 , 2021.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor akiagana  na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Hafez Ghanem mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao yaliofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma Septemba 28 , 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...