Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) Nahsoni Sigalla akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunga mafunzo ya maafisa uvuvi kwa ajili ya Sensa itakayoanza hivi karibuni kwa nchi nzima kwa vyombo vidogo vya majini.
Mshiriki wa mafunzo afisa Uvuvi, Maengo Nchimani akizungumza kuhusiana na mafunzo hayo ya namna watakavyochukua sensa kwa kisasa.


*Yabainisha matokeo ya sensa katika kufikia uchumi wa bluu na usalama wa vyombo hivyo.

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv, Bagamoyo 
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuanza kufanya sensa ya vyombo vidogo vya usafiri majini kwenye  maziwa,mito pamoja na bahari ili kuweka kanzidata ya kupanga maendeleo na usalama  katika sekta hiyo.

 Sensa hiyo itashirikisha  Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) pamoja na Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambapo sensa hiyo itaanza Oktoba Mosi hadi Oktoba 30 mwaka huu na kutambua idadi ya vyombo hivyo na shughuli zake. 

Akizungumza wakati wa semina ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa uvuvi na maafisa wa TASAC, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ambaye ni  Mkurugenzi Udhibiti Uchumi wa Shirika hilo  Nahson Sigalla amesema sensa hiyo ya nchi nzima pamoja na mambo mengine imelenga kuinua maendeleo ya sekta hiyo kusaidia katika utungaji sera za kiudhibiti.

Amesema sensa hiyo ni  mpango wa maendeleo pia itasaidia kuhimarisha usalama uhai na mali za watumiaji na wamiliki  wa vyombo hivyo nchini kote.

Sigalla amesema msingi wa  sensa ya vyombo hivyo itakayofanywa katika maeneo ya bahari, maziwa na mito ikijishughulisha na kazi za uvuvi, ubebaji wa mizigo pamoja na usafirishaji wa abiria itasaidia kutambua idadi ya vyombo hivyo na majukumu yake na baadae taarifa zake kuwekwa katika kanzidata maalumu.

"Tanzania inatekeleza uchumi wa bluu unaohusisha masuala yote ya uchumi wa bahari, imani tunayoijenga  kupitia sensa hii itatuwezesha kuona ni hatua zipi zichukuliwe kufanikisha maendeleo yake na kutatua changamoto zilizopo zinazokabili sekta hiyo" amesema Sigalla.

Aidha, amesema kwa kuzingatia utaratibu uliopo, sensa hiyo itavishirikisha vyombo vidogo vyenye urefu usiopungua urefu wa mita 24 na uwezo wa kubeba mizigo isiyozidi tani 50 katika maeneo yote ya ukanda wa bahari, maziwa na mito ambapo shughuli ya usafiri huo unahusika.

Amesema pamoja na kusaidia kupanga shughuli za kimaendeleo, sensa  ya vyombo hivyo pia itawasaidia wataalamu wa vyuo vya elimu ya juu  kufanya utafiti wao kuhusu uwepo wa vyombo hivyo kwa kuona kwa kiasi gani vinasaidia katika ukuaji wa maendeleo nchini wa dhamira ya Serikali ya uchumi wa bluu.

Sigalla alisema dhima nyingine ya sensa hiyo imetokana na mahitaji ya kitaifa ya upatikanaji wa taarifa hizo kwa ajili ya kuona njia sahihi kusaidia ukuaji wa maendeleo ya sekta hiyo inayotoa huduma zake katika maji.

Mmoja wa walengwa wa mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa Uvuvi kutoka Mkoa wa Kagera Maengo Nchimani amesema matarajio mafunzo hayo yatawasaidia  kufanikisha malengo yaliyokusudiwa huku akiamini ujio wake ni muhimu katika kuharakisha maendeleo ya taifa. 

Nchimani amesema  kumekuwepo na vyombo vingi vinavyotoa huduma ya usafiri na ubebaji wa mizigo katika mito, maziwa na bahari huku akiwataka wamiliki wa vyombo hivyo kutoa ushirikiano wa dhati sensa itakapoanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...