NA TIGANYA VINCENT

HALMASHAURI ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 884 ambayo ni sawa na asilimia  18 ya makadirio ya kukusanya bilioni 4.6.

Takwimu hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi |Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Dkt. Peter Nyanja wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema makusanyo hayo ni miezi miwili ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha unaoendelea.

Dkt.Nyanja alisema lengo lao ni kuhakikisha kabla ya kumalizika kwa robo ya kwanza wawe wamekusanya asilimia 25  ya makisio na kufikia bilioni 1.1.

Alisema mafanikio hayo yameanza kuonekana baada ya kubadilisha Watumishi waliokuwa wakihusika na ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuongeza nguvu ya ukusanyaji kwa kubuni vyanzo vipya.

Dkt.Nyanja aliongeza kuwa mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha huu wanatarajia kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ya kiasi cha milioni 100.

Aidha Dkt.Nyanja amevitaka vikundi vinavyokopeshwa fedha kuhakikisha vinazitumika katika kuimarisha mitaji yao ili wawaachie fursa watu wengine kunufaika na mikopo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhan Kapela (kulia)  akizungumza na waandishi wa habari leo. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda(kushoto) na Katikati ni Mkurugenzi Mteandaji wa Manispaa ya Tabora Dkt.Peter Nyanja
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo. Wengine ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhan Kapela (kushoto)  na Mkurugenzi Mteandaji wa Manispaa ya Tabora Dkt.Peter Nyanja
Mkuruenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Dkt. Peter Nyanja akizungumza na waandishi wa habari leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...