Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamasha la Michezo kwa wanawake litakalofanyika katika viwanja vya Uhuru na Mkapa kuanzia siku ya kesho Septemba 16 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbas amesema kauwa Mh. Rais atazindua tamasha hilo la siku tatu ambalo litashirikisha Michezo mbalimbali kwa wanawake.
“Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kuzindua tamasha la kwanza la Michezo la Tanzanite siku ya Jumamosi lenye lengo la kuitangaza nchi kupitia sekta ya Michezo ambalo Michezo na burudani mbalimbali zitakuwepo,” amesema Dkt. Abbas.
Dkt. Abbas amesema kuwa tamasha hilo litaanza kwa kutoa mada mbalimbali siku ya kesho zenye lengo la kuongeza uelewa wa umuhimu wa ushiriki wa Michezo kwa wanawake na kufuatiwa na Michezo tofauti katika viwanja vya Uhuru na Mkapa.
“Mheshimiwa Rais akiwa jijini Mwanza akizungumza na vijana alisisitiza sana juu ya sekta ya Michezo hapa nchini na kurudisha Michezo mashuleni na tunategemea kupitia tamasha hili tunatarajia kupata vijana wengi wenye vipaji,” amesema Dkt. Abbass.
Aidha Dkt. Abbass ameongeza kuwa tamasha hilo la siku tatu litakuwa ni la bure na hivyo kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujionea burudani mbalimbali za Michezo zitakazotolewa na wanawake.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...